Featured Post

KIAMA CHA BLOGU NA TV ZA MTANDAONI KIMEFIKA, LAZIMA WOTE WASAJILIWE. KESI YA WADAU WA HABARI YATUPILIWA MBALI

Wamiliki wa vyombo vya usambazaji habari kama vile blogu, TV na redio za mitandaoni nchini Tanzania wametakiwa kujisajili na kufuata maadili kwa mujibu wa kanuni husika.

Hatua hiyo inajiri baada ya serikali kushinda kesi iliofunguliwa na wadau wa habari kupinga kanuni za maudhui mitandaoni 2018.
Kulingana na taarifa hiyo iliochapishwa na mkurugenzi wa idara ya habari na maelezo na msemaji mkuu wa serikali Daktari Hassan Abbasi, walalamishi waliwasilisha maombi ya kupata ridhaa ya kufungua shauri la kufanyiwa marejeo kanuni hizo zilizosainiwa na waziri mwenye dhamana ya habari ambazo pamoja na mambo mengine zinasimamia zinasimamia usajili na kuweka mfumo wa uwajibikaji na maadili kwa wamiliki wa mitandao ya kijamii inayohusika na habari.
Katika kesi hiyo, serikali iliweka pingamizi tatu za kisheria ambapo pamoja na mambo mengine iliomba mahakama kutupilia mbali maombi hayo kwa kuwa walalamishi hawakuthibitisha kuwa wana haki ya kikatiba ambazo zitavunjwa na kanuni hizo, hoja ambazo zilikubaliwa na mahakama kuyatupilia mbali maombi hayo.
''Kwa hukumu hiyo , tunatumia fursa hii kuutarifu umma kuwa sasa wamiliki wa mitandao ya kijamii inayohusika na usambazaji wa habari kama blogu, TV na redio za mitandaoni na wengine walioainishwa katika kanuni wanapaswa kuendelea kujisajili na kufuata maadili kwa mujibu wa kanuni husika'', ilisema serikali katika taarifa hiyo.
Serikai ilisema kuwa wale wanaotuma maombi watahitajika kuwasilisha stakhabdhi zao ikiwemo maelezo ya hisa, uraia, kibali cha kuonesha wanalipa kodi mbali na mipango ya mafunzo.
Wanablogu ambao wataopatikana na hatia ya kutoheshimu sheria hizo mpya watakabiliwa na faini ya hadi milioni 5 ama kifungo kisichopungua miezi 12 ama zote mbili kulingana na sheria hizo mpya, ilisema taarifa hiyo.
Rais Magufuli alitoa agizo la kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote atakayechapisha habari za uongozi kuhusu serikali katika mitandao ya kijamii.

Idadi ya watumiaji wa mitandao nchini Tanzania ilipanda hadi asilimia 16, 2017.

Comments