Featured Post

ZITTO, USIZIFANYE TUHUMA ZA NONDO KUWA ZA KILA MZAWA WA KIGOMA



Na Moses Machali
KWANZA nianze kwa kusema kwamba uhamiaji kumshuku na kumtuhumu  mtu kuwa siyo raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuamua kumuhoji ni sehemu ya wajibu wao.

Na ni ujinga kuwaaminisha watu wote kwamba mkazi mmoja au mzawa yeyote wa Mkoa wa Kigoma akituhumiwa na uhamiaji kuhusu uraia wake au kwa kosa lolote basi tuhuma hizo ni wazawa wote wa Mkoa wa Kigoma.
Kufanya hivyo siyo sahihi kwa namna yote iwavyo kwa sababu wapo watanzania wengi wameowahi kutuhumiwa kuwa siyo Raia kisha wakathibitika ni raia na wakaachwa huru.
Kwa mujibu wa sheria ya Uhamiaji ya Mwaka 1995 chini ya kifungu cha 7 (d) “Without prejudice to the generality of section 6, and for the purpose of the better administration of this Act, any immigration officer may- if he has reasonable cause to suspect that any person has contravened any of the provisions of this Act or of any regulations made here-under or that the presence in Tanzania of any person is unlawful, and if he is of opinion that in order to prevent justice from being defeated it is necessary to arrest such person immediately arrest any such person without warrant, and such person shall be brought before a magistrate as soon as is practicable.”
Kifungu hicho kinawapa maafisa Uhamiaji haki ya kumkamata na kumuhoji mtu yeyote ambaye wana mashaka naye kuwa yupo nchini kinyume cha sheria.
Aidha, tuhuma za Uhamiaji dhidi ya mtu yeyote kuhusu uraia wake siyo za mwisho bali raia ambaye ataona kaonewa bado ana nafasi ya kukata rufaa kwa mamlaka nyingine kwa mujibu wa sheria hii ya uhamiaji, yaani The Immigration Act, 1995.
Kwa hiyo Zitto na wenzake ambao wanaweza kuwa wanalitumia suala la Abdul Nondo kisiasa kwa manufaa yao ya kisiasa waache kulifanya kuwa ni dhambi Uhamiaji kumtaka Nondo kuthibitisha iwapo ni raia au siyo raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu ni sehemu ya wajibu wao Uhamiaji kutuhumu kwa haki na kufanyia kazi tuhuma zote kwa haki.
Iwapo Abdul Nondo atathibitisha ni raia ataachwa huru kama wewe zitto ilivyowahi kuachwa huru.
Nondo siyo wa kwanza kutuhumiwa na wala wewe Zitto haukuwa wa Kwanza Kutuhumiwa na wala haiwezekani Nondo akawa wa mwisho kutuhumiwa kwa sababu dunia ina watu wengi na walimwengu hao wanaweza kuhamia ktk nchi yetu kiharamia na kusababisha matatizo ya kisiasa; kiuchumi; na kijamii na kwa hiyo lazima Uhamiaji wapewe meno ya ku-dili nao kwa ku- establishi tuhuma dhidi yao kwa haki huku wale watakaothibitika tuhuma haziwahusu wataachiwa huru.
Sasa Zitto kwa nini unawapiga mkwara Uhamiaji waache kutimiza moja ya wajibu wao kwa mujibu wa sheria na kutaka kulifanya suala la Nondo ni issue ya watu wote wa Mkoa wa Kigoma?
Ningesema unafanya uzwazwa lakini nakustahi kama kaka lakini siwezi acha kusema ni ujinga wa kiwango cha juu.
Mhe. Zitto, mbona haukuwahi kulifanya suala la Bashe kuwa la Watanzania wote mwaka 2010 au kwa sababu Bashe ni mwanachama wa CCM?
Mnamtumia Nondo vibaya na sasa anaharibikiwa kwa sababu ya uchanga wake kifikra.
Nondo hana maarifa mapana kuhusu Siasa za Kikanjanja, na hajui kwamba wapo wanasiasa wanaweza kuwatanguliza vijana mbele halafu watakapoharibikiwa watabakia wao kama wao na hatimaye future zao zinaenda kombo.
Waswahili husema kuwa uyaone na akili za kuambiwa changanya na zako. Nondo hajachanganya na zake bali kaona atapata umaarufu kwa kutumika vibaya kama inavyodhaniwa.
Vijana kama akina Philipo Mwakibinga ni maadhura wa siasa kanjanja kama anazofanyiwa Nondo leo hii. Mwakibinga na wengine wengi waliokuwa wakisoma vyuo vikuu mbalimbali walipoteza fursa za kuhitimu masomo yao ya chuo kikuu huko UDOM; UDSM, NK.
Hata mimi niliwahi kunusurika nikiwa nafanya shahada yangu ya kwanza kule SAUT mwanza, bahati nzuri niliachwa kwa kuwa nilikuwa nimebakiza mtihani mmoja wa kuhitimisha muhula wa mwisho kabisa wa elimu yangu ya shahada ya kwanza.
Ilibakia Kidogo Cahdema iniponze. Vinginevyo kwa mujibu wa Mwadili wa wanafunzi yaani Dean Of Students kwa zama zile ningeonja joto la jiwe kama walivyoonja akina Philipo Mwakibinga kule UDOM.
Ndiyo maana nasema kijana kama Nondo anaponzwa na ufinyu wa maarifa kuhusu wanasiasa makanjanja ambao huwatumia wakati wakiwa na shida nao lakini dude likiamshwa hubakia peke yao na janga watalikabili wenyewe vijana kama Nondo.
Vijana acheni kuvimbishwa vichwa halafu mnajiona wanasiasa kanjanja wanawajali kwa sababu mwisho wa siku watawaacha solemba yaani mtabikia na majanga yenu huku wakiishia kusema poleni sana na ndiyo harakati za ukombozi. Kijana  jiulize hayo maneno yanakusaidia nini?
Mhe. Zitto, Historia inaeleza kuwa hata Jenerali Ulimwengu aliwahi kuhojiwa na Uhamiaji.
Wengine ni akina Husein Bashe Mbunge wa Nzega; Wallace Karia Rais wa sasa TFF; wewe Mwenyewe Zitto Kabwe; Hezekia Wenje aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana; na watu wengine mashuhuri na wasio mashuhuri wana CCM na wasio wana CCM wamekuwa wakituhumiwa na kuhojiwa na mamlaka za nchi.
Haikuwahi kutokea mtu yeyote kutaka kuzifanya tuhuma hizo kuwa ni za wakazi wote wa mkoa wowote ule au ni tuhuma na dharau kwa watu wa mkoa wowote ule au dharau kwa wananchi wote wa taifa hili.
Ndiyo maana nasema ni ujinga wa kiwango cha juu kwa mtu mweledi na mjumbe wa Bunge linalotunga sheria unayeelewa fika kwamba sheria inawapa haki maafisa wa uhamiaji kumuhoji na kumtaka mtu yeyote kuthibitisha au kutoa taarifa zake kuhusu uhalali wa uraia wake.
Kwa hiyo Nondo ni mtu kama watu wengine ambao wamewahi kutuhumiwa.
Hakuna sababu ya kulifanyia siasa suala la Bwanamdogo huyo ili kujipatia kiki kisiasa. Kama anaonewa itafahamika tu na ataachiwa huru.
Waache Uhamiaji wafanye kazi yao. Nawe kama una maelezo ya ziada kuhusu uhalali wa Nondo basi saidia kuthibitisha hilo badala ya kutaka kwamba kila mtu wa Kigoma aone tuhuma za Nondo ni za kwake wakati sivyo ilivyo.
Nondo amaetuhumiwa yeye kama yueye na hivyo sisi wazawa wengine wa Kigoma hatujatuhumiwa kama unavyotaka ionekane.
Aidha, usitake kuaminisha watu kwamba wanaothumiwa ni wazawa wa Kigoma tu. Jiulize Hivi Bashe ni mzawa wa Kigom? Wallace Karia Rais wa sasa wa TFF ni mzawa wa Kigoma? Sijui mkoa aliozaliwa Mzee Jenerali Ulimwengu lakini nafikiri siyo mzawa wa Mkoa wa Kigoma, nk.
Je, kwa nini unafanya propaganda kwamba wanaotuhumiwa ni watu wa kigoma pekee?
Unawakosea Uhamiaji kwa kutaka kuwazuia wasifanye kazi yao jambo ambalo linaweza kuwa kosa kisheria pia.
Nakutakia kazi njema na busara itamalaki kichwani mwako na katika roho yako kaka na wengineo wanaopotosha suala hilo.

Comments