Featured Post

TIMU ZAPUNGUA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MEI MOSI MKOANI IRINGA


Makamu Mwenyekiti wa kamati ya michezo ya mei mosi kitaifa Joyce Benjamin akitoa kero ya kamati ya mashindano ya mei ya mosi taifa inasikitishwa na kupungua kwa timu shiriki katika mashindano hayo yanaendelea mkoa wa Iringa kutoka timu kumi na Tano (15) mwaka jana hadi timu kumi (10) mwaka huu 2018 mbele ya katibu tawala msaidizi mkoa Majuto Njanga  aliyekuja kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza. 


Viongozi mbalimbali wa michezo ya mei mosi wakiwa jukwani  wakipokea maandamano ya timu shiriki zilizokuwa zikiingia uwanjani
Timu ya uchukuzi na timu nyingine zikiingia uwanjani  
 Baadhi ya viongozi na wadau wakiwa jukwaani wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mei mosi katika uwanja wa kumbukumbu ya Samora  

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

KAMATI ya mashindano ya mei ya mosi taifa inasikitishwa na kupungua kwa timu shiriki katika mashindano hayo yanaendelea mkoa wa Iringa kutoka timu kumi na Tano (15) mwaka jana hadi timu kumi (10) mwaka huu 2018.

Kauli hiyo imetolewa na makamu mwenyekiti wa kamati ya michezo ya mei mosi kitaifa Joyce Benjamini wakati wa uzinduzi wa michezo ya mei mosi kwenye kiwanja cha kumbuku ya Samora Mkoani Iringa.

Benjamini alisema kuwa kupungua kwa idadi ya timu shiriki kunatokana na baadhi ya mashirika ya sekta ya UMMA na serikali kushindwa kupeleka timu kwa visingizio vya ukata ili hali timu ya Rais ikiwa imeshiriki mashindaano hayo.

“Mheshimiwa mkuu wa mkoa tunapenda kutoa malalamiko yetu juu ya kupungua kwa hizi timu na kusingizia ukata wa pesa jambo ambalo sio kweli kwa kuwa waziri mkuu,makamu wa rais na rais wetu ni viongozi wapenda michezo hivyo uoga wao ndio umefanya kushindwa kuzileta timu zao zishiriki mashindano haya” alisema  Benjamini

Benjamini alisema kuwa hakuna mahali ambako rais amekataza wafanyakazi wa serikalini kutoshiriki michezo mbalimbali,viongozi wetu wa serikali wamekuwa waoga kwenye matumizi ya fedha za serikali,anachokitaka Rais ni uhalisia wa matumizi ya fedha katika maeneo husika.

“Mhesmimwa mkuu wa mkoa hata ukiangalia kwenye ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 hadi mwaka 20102 ibara ya 61 ukurasa wa 218 hadi 219 unasema wajuu ya kuinua na kuendeleza michezo hapa nchini,sasa kwanini viongozi hawafuati ilani hiyo” alisema  Benjamini

Benjamini alizitaja timu zinazoshiriki mashindano hayo mkoani Iringa kuwa ni timu kutoka Ofisi ya Rais –Ikulu,Wizara ya Uchukuzi,Chuo Kikuu kishiriki cha Afya na sayansi (MUHAS),Hifadhi za Ngorongoro,Geita gold mine (GGM),Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA),Shirika la umeme Tanzania (TANESCO),Tumbaku-TTPL ya Morogoro,Ukaguzi na Wenyeji timu ya RAS Iringa.

“Hizo ndio timu zilifika kwenye kituo hiki mkuu lakini nichukue nafasi kuzitaja timu ambazo zimenipa simanzi ya kutoshiki mashindano haya ni kama vile timu ya Ofisi ya Waziri mkuu,Wizara ya Mambo ya Ndani,Maliasilina Utalii,Wizara ya afya maendeleo ya jamii,timu za mashirika ya UMMa kama TTCL,Posta,Bima,NSSE na nyingine nyingi ambazo zilikuwa washirika wazuri wa michezo ya mei mosi” alisema

Akizungumza kwa niamba ya mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza, katibu tawala msaidizi mkoa Majuto Njanga amezionya timu ambazo zinashiriki kwenye michuano ya mei mosi kuacha kuchukua wachezaji ambao sio wafanyakazi kwani kufanya hivyo kunapunguza ladha ya mashindano hayo.                                

Njanga alisema kuwa michezo hujenga undugu na furaha baina ya wanamichezo hivyo kuwaingiza wachezaji ambao sio wafanyakazi kwenye mashindano hayo wataondoa maana halisi ya mashindano hayo jambo ambalo linaweza kuwafanya kushindwa kufikia malengo yao waliojiwekea. 


“Mashindano haya ni ya wanamichezo wafanyakazi,kuna wale wanamichezo ambao sio wafanyakazi ambao wanajulikana kama mamluki au wavamizi kwamba hapa sio mahala pao nawasihi tuchezeshe wafanyakazi halisi ili mshindi apatikane kihalali na sio vyenginevyo kwa sababu ni hatari sana kumleta mwanamichezo ambaye sio mfanyakazi kwenye michezo hii anaweza kuvunjika mguu au akifa kwa mfano hatuombei itokee hiyo itakuwaje “Alisema Njanga 

Aidha Njanga alizitaka timu hizo kuacha kuwatumia wachezaji wa aina hiyo kwani wana madhara makubwa hasa pale yanapokuwa yakijitokeza kwa kuzitaka timu zenye utamaduni huo kuhakikisha wanaondokana nao. 
  
Hata hivyo Njanga alionekana kukerekwa na baadhi ya menejimenti za Taasisi,Mashirika na makampuni mbalimbali kuwa na utashi wa kutokupenda michezo na wengine kwa kisingizio cha ukosefu wa fedha kuacha kufanya hivyo badala yake wamuunge mkono Rais Jakaya Kikwete katika jitihada zake za kuinua na kuendeleza michezo hapa nchini. 

Akizungumzia waamuzi wanaochezesha mashindano hayo, Njanga aliwataka kuchezesha kwa haki bila upendeleo kwa kufuata sheria za mchezo husika ili mshindi aweze kupatikana kihalali kwa sababu wakienda kunyume chake wanaweza kusababisha tafrani na manung’uniko kwa baadhi ya timu shiriki. 

Hali kadhalika aliwataka kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya hali ya juu wakati wote wa mashindano ikiwemo kukubaliana na matokeo pindi watakapojikuta wamefungwa wakati wa mashindano hayo. 

Comments