Featured Post

MSIMSHANGAE RAIS MAGUFULI, NI BINGWA WA MIUNDOMBINU


Na Daniel Mbega
BINAFSI nimefanikiwa kuizunguka Tanzania Bara kwa kiwango kikubwa kwa miaka zaidi ya 25 nikiwa katika shughuli mbalimbali za kihabari na hata kibinafsi, zaidi nikitumia njia ya reli na barabara.
Ninaifahamu Tanzania Bara ile ya wakati tukitumia siku tatu kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kwa kulazimika kupitia Nairobi nchini Kenya wakati safari yetu ni ya humu ndani.

Au wakati tukisafiri kwa siku tatu kutoka Dar es Salaam hadi Sumbawanga mkoani Rukwa kwa sababu ya ubovu wa barabara.
Ninakumbuka namna ambavyo wananchi wa mikoa ya Kusini mwa Tanzania - Lindi na Mtwara - walivyokuwa wakitumia mpaka siku tano kuvuka katika Mto Rufiji!
Leo hii mtu akitaka kwenda Sumbawanga, hahitaji kutumia siku mbili kama ilivyokuwa zamani, bali atatumia siku moja tu kwa sababu kuna gari la moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Sumbawanga – umbali wa takriban kilometa 1,109.3 kwa siku moja badala ya mbili.
Wasafiri wa kwenda Mwanza, umbali wa kilometa 1,387.3, ambao zamani walitumia siku mbili, tena wakipitia katika nchi jirani ya Kenya ambako walilazimika kuwa na passport na viza, leo hii wanatumia saa 14 tu kutoka Dar es Salaam, wakati wale wa kwenda Kigoma na Kagera wanatumia siku moja na nusu tu badala ya siku tatu hadi nne za zamani.
Siyo hivyo tu, leo hii unasafiri kutoka Dar es Salaam hadi Mtwara kwa kutumia muda wa saa saba tu badala ya siku tano zilizokuwa zikitumika wakati ule barabara ilipokuwa mbovu pamoja na kivuko dhaifu.
Sasa unaweza kufika Lindi kwa saa tano tu kwa kuwa kwenye Mto Rufiji kuna Daraja la Mkapa lililowakomboa Watanzania wengi na adha ya usafiri.
Leo unaweza kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, au Dar es Salaam hadi Sumbawanga na hata ukatoka Mbinga hadi Dar es Salaam kwa siku moja tu, yaani usizidishe saa 24.
Hii ni kwa sababu kuna 'nyoka mweusi', yaani barabara zote ni lami, zinateleza tu bila shida.
Aidha, leo hii mtu anaweza kutoka Dar es Salaam kwenda Mbinga (kilometa kama 1,400) kwa siku moja kwani kuna basi la moja kwa moja kupitia Masasi hadi Songea kwa mwendo wa saa 14 tu.
Nimesafiri katika kipindi hiki kutoka Iringa kwenda Arusha kupitia Dodoma-Singida hadi Manyara; kutoka Dar es Salaam-Kiteto-Kondoa hadi Babati; nimepita Babati-Kondoa-Mayamaya hadi Dodoma; nimepita Mwanza-Shinyanga-Tabora-Mpanda hadi Sumbawanga mpaka Mbeya; nimetoka Dar es Salaam-Njombe-Songea hadi Mbambabay mkoani Ruvuma; nimetoka Mwanza-Musoma hadi Sirari; nimezunguka Mwanza-Sengerema-Geita hadi Bukoba.
Si hivyo tu, nimetoka Bukoba kupita Kahama hadi Dar es Salaam; nimetoka Shinyanga-Maswa-Bariadi hadi Lamadi; pia nimesafiri kutoka Dar es Salaam-Lindi-Masasi-Songea hadi Mbambabay na maeneo mengine mengi bila usumbufu wowote kwa kipindi kifupi tu.
Bado sehemu ndogo tu ya kutoka Kondoa hadi Babati ambayo inakamilika punde na baada ya hapo itakuwa ni lami tupu.
Ni maeneo machache tu ambayo bado hayajaunganishwa kwa lazimi ambapo miradi hiyo ilikuwa imekwama kwa sababu ya ukosefu wa fedha.
Huu ni mtandao mkubwa wa barabara zenye urefu wa kilometa 6,276.82 ambazo zilitiwa lami kwa gharama ya Dola 102,654.98 milioni.
Tunajivunia yote haya kwa sababu ya jitihada za Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kipindi cha miaka takriban 15 sasa, lakini lazima tuseme wazi kwamba, yupo mtu aliyekuwa ameaminiwa na serikali hiyo kusimamia miundombinu ya barabara.
Huyu si mwingine bali ni Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye anaendelea kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda sawa.
Utendaji wa Dk. Magufuli unajieleza wenyewe katika kipindi chake cha miaka 20 akiwa ndani ya Baraza la Mawaziri, na zaidi anafahamika namna alivyoisimamia vyema na kwa mafanikio makubwa Wizara ya Ujenzi (Miundombinu) ambapo katika kipindi alichokaa kwenye wizara hiyo alifanikiwa kusimamia miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara.
Pamoja na kutokamilika kwa baadhi ya vipande hivyo, ambavyo kwa sasa vimeanza kutengenezwa ili kuikamilisha miradi hiyo, lakini leo hii unaweza kuizunguka Tanzania Bara bila shida tofauti na miaka ya nyuma.
Mtakubaliana nami kwamba, juhudi za Dkt. Magufuli katika kuimarisha mtandao wa barabara nchini umeipa nguvu Serikali ya CCM na hakuna mtu anayeweza kubeza hilo.
Chini ya Dkt. Magufuli barabara zilizojengwa kwa kiwango cha lami ni pamoja na: Singida-Iguguno (76km); Sekenke-Shelui (33km); Mwandiga-Manyovu (60km); Kigoma-Kidahwe (35.7km); Bonga-Babati (19.20km); Tabora-Urambo (42km); Kyaka-Bugene (59.1km); Dareda-Minjingu (84.6km); Kidahwe-Uvinza-Ilunde (76.6km); Isaka-Ushirombo (132km); Kilwa Road Phase III (1.5km); Nyanguse-Musoma (85.5km); na Kagoma-Lusahunga (154km ).
Nyingine ni Isuna-Singida (63km); Tarakea-Rongai-Kamwanga (32km); Iringa-Migori (95.1km); Migori-Fufu Escarpment (93.8km); Nangurukuru-Mbwemkuru (95km); Shelui-Nzega (112km); Kyamorwa-Buzirayombo (120km); Manyoni-Isuna (54km); Arusha-Namanga (104.2km); Chalinze-Tanga Phase I (125km); Daraja la Umoja (10.7km) linalounganisha Tanzania na Msumbiji; Sengerema-Usagara (40km); Buzirayombo-Geita (100km); Geita-Sengerema (50km); Dodoma-Mayamaya (43.65km); Manyoni-Itigi-Chaya (89.3km); Puge-Tabora (56.1km); Handeni-Mkata (54km); Korogwe-Handeni (65km); Katesh-Dareda (73.8km); Singida-Katesh (65.1km); Tanga-Horohoro (65km); na Peramiho Junction-Mbinga (78km).
Barabara nyingine ni Sam Nujoma jijini Dar es Salaam (4km); Magole-Turiani (48.6km); Tabora-Urambo (52km); Dumila-Rudewa (45km); Mbeya-Lwanjilo (36km); Lwanjilo-Chunya (36km); Mwigumbi-Maswa-Bariadi-Lamadi (71.8km); Nzega-Puge (58.8km); Fufu Escarpment-Dodoma (70.9km); Sumbawanga-Kanazi (75km); Kanazi-Kizi-Kibaoni (76.6km); Sumbawanga-Matai-Kasanga (112km); Ikana-Laela (64.2km); Masasi – Mangaka Phase I (15km); Masasi – Mangaka Phase II (17.6km); Masasi – Mangaka Phase III (22.5km); Dodoma – Manyoni (127km); Barabara ya Kilwa Phase II (5.1km); Tinde – Mpaka wa Shinyanga/Mwanza (96km); Nzega-Tinde-Isaka (73km); Morogoro – Dodoma (256km); Marangu – Rombo Mkuu (32km); Rombo Mkuu – Tarakea (32km); Barabara ya Mandela (15.6km); Tabora – Nyahua – Chaya (85km); Ushirombo – Lusahunga (110km); Namtumbo – Kilimasela Lot A (60.7km); Matemanga – Tunduru Lot C (58.7km); Kilimasela – Matemanga Lot B (68.2km); Iyovi-Iringa-Mafinga (149.6km); Laela – Sumbawanga (95.31km); Chalinze – Tanga Phase II (120km); Tanga Magharibi PMMR (224.8km); Tanga Mashariki (116.8km); Ndundu – Somanga (60km); Mbwemkuru – Mingoyo Lindi (95km); Arusha – Minjingu (98km); Songea – Namtumbo (67km); Tunduma – Ikana (63.2km); Mkuranga – Kibiti (60km); na Bagamoyo – Msata (64km).
Hivi sasa kuna miradi mingine ya barabara ambayo inaendelea kufanyiwa pembuzi yakinifu na nyingine zimekwishapata wakandarasi kwa ajili ya ujenzi.
Tunafahamu kuhusu ujenzi wa barabara za juu pale Tazara na Ubungo ambao unaendelea na kukamilika kwake kutasaidia kubadili sura ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na kupunguza msongamano wa magari.
Hakuna shaka yoyote kwamba mafanikio haya ni makubwa na tunahitaji kuunga mkono jitihada hizi za serikali kwa maendeleo ya Watanzania wote.
0656-331974

Comments