Featured Post

KUMBUKUMBU ZANGU NA MWEZI APRILI



NA CONGES MRAMBA, MWANZA
APRILI tulikumbuka vifo vya watu mashuhuri sana hapa duniani wenye nasaba na Bara la Afrika.
Ndiyo mwezi aliokufa Hayati Edward Moringe Sokoine, William Tolbert wa Liberia, Martin Luther King Jr, na mashujaa wengine wengi.
Nianze na kifo cha Tolbert huko Liberia.
Samuel Kanyon Doe alizaliwa Mei 6, 1951, akaja kuuawa kinyama  Septemba  9, 1990.
Aliongoza Liberia kuanzia mwaka 1980 hadi 1990.
Alizaliwa katika mji mdogo wa Tuzon, katika Kaunti (County) ya Grand Gedeh, Kusini Mashariki mwa Liberia.

Wazazi wake walikuwa fukara wasio na elimu kama ilivyo watu wengi wa vijijini huko Liberia au hata hapa kwetu Tanzania.
Alikuwa kutoka kabila la Krahn, watu maskini na wasio na elimu.
Wakati huo, ni yeye pekee aliyehitimu shule ya msingi, akaingia jeshini kwa kuwa hakukuwa na nafasi nyingine ya kazi.
Oktoba 1979 ndipo alipopata cheo cha ‘Master Sergeant’ katika Jeshi la Liberia.
Akawa anajisomea usiku masomo ya ‘High School’ ndipo wakati huo yeye na vijana wenzake 17 walipompindua Rais.
Huu ndio ulikuwa mwanzo wa mapinduzi dhidi ya William Tolbert.
Walimkamata Rais William R. Tolbert Jr, wakasimika utawala wa kijeshi, hiyo Aprili 12 mwaka 1980.
Tolbert na Sokoine walikufa Aprili 12.
Sokoine alikufa kwa kile kinachosemwa ajali ya gari mwaka 1984, wakati Tolbert aliuliwa Aprili 12 mwaka 1980 na wanajeshi waliopindua serikali.
Rais Tolbert (66) aliongoza Liberia iliyokuwa tulivu sana, “The Model of Peace in Africa” zama hizo.
Alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU) wakati anapinduliwa.
Uenyekiti huo alipewa wakati wa Mkutano wa 16 mjini Monrovia.
Mauaji ya Tolbert yalifanyika Aprili wakati wa Pasaka, ndiyo maana yanaitwa “Blood Easter”.
Wenzake, Brigedia Jenerali Abraham Kollie, Tom Quiwonkpi, Thomas Weh Sen (alikuwa Makamu Rais wa Doe) alichinjwa mwaka huo huo, Nicholas Podier alitimuliwa jeshini!
Maiti ya Tolbert na watu wake 27 waliouawa wakati wa mapinduzi hayo ya kijeshi, zikazikwa katika makaburi mawili ya pamoja mjini Monrovia. Maiti zote zilisombwa kwa lori!
Kwa hiyo, Doe yeye alikuwa msomi miongoni mwa vijana 18, akawa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Ukombozi, lililoitwa People’s Redemption Council (PRC).
Tunajua licha ya kumuua Rais, aliwachinja wafuasi wake baada ya mapinduzi hayo. Katiba ikabadilishwa, ukawa utawala wa kijeshi, yaani "military junta.”

DOE KIBARAKA WA MAREKANI
Doe wakati huo alihitilafiana na msimamo wa Rais wetu, Mwalimu Nyerere juu ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, na siasa zetu za kutofungamana na upande wowote katika Vita Baridi (Cold War), ila sisi vijana tulimhusudu tu Doe.
Liberia ina watumwa wa zamani huko Marekani, wanajiita, “Americo-Liberian elites” waliorejea kuanzisha taifa hilo mwaka 1847, sasa yeye alitoka kabila dogo tu.
Doe, aliwaruhusu Wazungu kufanya lolote Liberia, hata makampuni na mimeli yao haikutozwa kodi.
Wazungu walishiriki misamaha ya kodi Liberia, walishiriki ufisadi mkubwa, mimi na vijana wenzangu tukiihusudu tu picha ya Doe.
Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) ndilo liliwasaidia kufanya unyama mkubwa Liberia, na inasemwa alikuwa shushushu wa CIA aliyemlipua Tolbert.
Ilitangazwa mwaka 1989 kwamba Doe alihitimu Shahada ya Kwanza (BA) hapo Chuo Kikuu cha Liberia.
Doe alikuwa mtambo wa kuwakata kilimilimi waliounga mkono Ukomunisti wa Kirusi na Cuba zama hizo.

CHARLES TAYLOR
Aliyeondoa mzizi wa fitina ni Charles Taylor (sasa mfungwa wa maisha) aliyeingia kutoka Ivory Coast na wapiganaji wa msituni Desemba 24, 1989.
Taylor alitoroka jela Marekani (wakati mwingine inasemwa alitoroshwa na CIA) akaenda Libya kwa Gaddafi, akafundishwa vita, akaja sasa kumpinga Doe, maana Marekani wakikutumia sana wanakuua kwa kukugonganisha vichwa na wenzako, wao wakiwa pembeni wanatazama!
Mwaka 1990 nchi ilikuwa msambweni, Doe alikamatwa mjini Monrovia na Prince Y. Johnson  Septemba 9, 1990.
Alikuwa akihudhuria mkutano wa ECOMOG, Jeshi la Kulinda Amani huko Magharibi mwa Afrika.
Makao Makuu yalikuwa Monrovia, sasa Johnson alikuja na majeshi yake, akamkamata Doe, baada ya vita kali ya bunduki. Ilikuwa ‘Ambush’.
Jamaa alichukuliwa mateka, akapelekwa katika ngome ya Johnson, akateswa sana; alitembezwa uchi wa mnyama mjini Monrovia akiwa uchi wa mnyama, watu wakishangilia sana kutokana na unyama wake.
Ni hawa hawa Marekani waliomuua Mweusi mwingine, Malcolm X na Martin Luther King Jr.
El-Hajj Malik El Shabazz, ni Mwanaharakati maarufu wa Haki za Weusi wa Marekani, ambaye wakati dunia inapojadili ukandamizaji wa Weupe dhidi ya Weusi wa Marekani, hatasahaulika.
Malik El-Shabazz, ambaye ni maarufu sana duniani kama Malcolm X alikuwa Mwamerika  Mweusi, tena Kiongozi wa Dini ya Kiislam aliyezaliwa Mei 19, 1925 Kaskazini mwa Omaha, Nebraska, Marekani.
Mwanaharakati huyu aliuawa Feburuari 21, 1965 huko New York.
Aliwahi kumwoa kidosho mmoja aitwaye Bety mwaka 1958 hadi alipofariki mwaka huo 1965, akazaa watoto Qubilah, Ilyasah, Malikah, Malaak, Gamilah, Lumumba na Atallah.
Familia ya mtu huyu iliishi katika vitisho na majaribio ya mauaji ya kila mara.
Feburuari 14, 1965 familia hii ilinusurika kuuawa mjini New York, lakini hakuna mtu aliyeshitakiwa kwa kosa la jaribio la mauaji ya watu hawa.
Hatimaye, siku saba baada ya jaribio hili yaani Feburuari 21 huko Manhattan, wakati Malcolm akihutubia, watu watatu wakiwa na silaha walikuja upesi wakampiga risasi huku wakiwa karibu naye.
Walimfyatua risasi mara 15.
Alipelekwa Hospitali ya Presbyterian akafariki baadaye akiwa na umri wa miaka 39.
Ibada ya mazishi yalifanyika Feburuari 27, 1965 katika Hekalu la Kikristo na yalihudhuriwa na jumla ya watu 1,600 akazikwa makaburi ya Femcliff huko Hartsdale, New York.
Baadaye mwaka huo, mkewe Betty alizaa mapacha wawili.
Inakisiwa, mtu huyu aliuawa na vikosi vya Usalama, hususan Federal Bureau of Investigation (FBI), na miaka mitatu baadaye, Aprili 1968, Martin Luther King Jr, naye aliuawa na Makao Makuu ya Jeshi la Marekani, The Pentagon.
Mtu huyu alizaliwa Januari 15, 1929, akaja kuuawa Aprili 4, 1968.
Alikuwa Mweusi, ndugu zetu waliopelekwa Marekani kama watumwa ili kulima mashamba ya mabwana wakubwa.
Alikuwa mwanaharakati aliyepinga ubaguzi na dhuluma.
Huyu ndiye aliyeiona ndoto ya Mweusi kutawala Marekani, “I Have A Dream” mwaka 1968, kabla ya kifo chake, na miaka 40 baadaye, Barack Obama akaja kuwa Rais mwaka 2008.
Ni maarufu kwa hotuba yake hii ya Ndoto ya Mweusi wa Afrika kutawala Marekani, akipanga vita dhidi ya Vietnam na umaskini wa Weusi na dhuluma waliyofanyiwa na ‘Magabacholi’ Wazungu.
Alitunukiwa tuzo ya Nobel Oktoba 14, 1964 kwa mtindo wake wa kupinga ubeberu bila kulipa kisasi, ‘nonviolence’.
Aliuliwa na Pentagon huko Memphis, Tannessee.

LINCOLN
Abraham Lincoln, Aprili 14, 1865 alipigwa risasi na John Wilkes Booth, mcheza sinema katika jumba la sinema, Ford’s Theater, Washington, akaja kufa Aprili 15.
Kawaulize waandishi wa habari waliandika nini kama siyo kwamba hawa viongozi walikufa kwa risasi na wauaji wakatajwa?
J.F. Kennedy alipouawa alisingiziwa Lee Harvey Oswald ambaye naye aliuawa na Jack Ruby wakati akisubiri kusikilizwa kesi yake.
Lincoln aliuawa na mashushushu wa Marekani, kama wengine, tena mwezi huo Aprili.
Martin Luther, yule Kasisi wa Katoliki, aliuliwa huko Ujerumani zama za Matengenezo ya Kikristo (Christian Reformation), yupo Martin Luther King Jr wa Marekani, Malcom X (Malik al Shabaaz) alipigwa risasi na  Ma-Jesuits  mwaka 1963, Bruce Lee,  mcheza filamu maarufu aliuliwa huko Hong Kong.

TITANIC
Nikusimulie kidogo kuhusu meli ya Titanic, ambayo hata BCBG wameimba juu yake.
Ilianza kujengwa 1909 huko Belfast, Ireland chini ya kampuni ya White Star.
Ilianza safari zake Aprili 10, 1912 iliongozwa na Kapteni E.J. Smith ambaye alipewa maelekezo kwenda Atlantiki kwenye mabonge ya barafu ili kuigongesha meli hiyo na kuua watu.
Tazama ni mwezi  Aprili.
Nataka nikwambie msomaji. Kulikuwa na matajiri wenye mali, wenye fedha nyingi. Mali zao zilikuwa za thamani ya Dola bilioni 12 ambao wote wangezamishwa Aprili 1912.
Hawa ni Benjamin Giggenheim, Isidor Strauss ambaye alikuwa Meneja wa Marcy’s Department Store, na John Jacob Astor.
Hawa walikuwa matajiri wa Kimarekani na walikuwa wapinzani wakubwa wa Ajenda ya Siri ya kuitawala dunia kwa nguvu ya pesa, nguvu ya utajiri, kupitia mabenki makubwa kama Benki ya Dunia (WB) na Fuko la Kimataifa la Fedha (IMF).
Nahodha wa Meli ya Titanic, E.J. Smith, alielekezwa kuizamisha meli ili kuwaulia mbali matajiri waliokuwemo.
Matajiri hawa walioangamia katika ajali hiyo  ni John Jacob Astor,Archibald W.Butt,Charles M. Hayes,na mkewe na binzi zao, W.T.Stead,Benjamin Guggenheim, F.D. Millett na G.D. Widher.
Wengine walioangamia ni Isidor Strauss, na mkewe, J.B Thayer, J. Bruce Ismay, Henry B. Harris na mkewe na Washington A. Roebling.
Sababu za kifo cha Rais J.F. Kennedy, ilikuwa Vita vya Vietnam, na siri waliijua Federal Reserve Bank.
Rais J.F. Kennedy alituma wapelelezi Vietnam, akina McNamara na Taylor, wakaleta Ripoti iliyomshauri Rais kuondoa majeshi Vietnam, akawakosea hawa mabeberu wa Ulaya na Marekani!
Waliazimu J.F. Kennedy aondoke wao waendeleze vita vya maslahi yao Vietnam.
Mwezi  Aprili hutufundisha mengi, ila nimeorodhesha wachache hawa ili tukumbuke unyama wa jamaa hawa ambao siku hizi tunawaona kama wahisani, na wana waandishi waliojivika maofisa habari wa Marekani hapa!
Kama wanaweza kuua hata rais wao, wewe Mweusi mbona wajipendekeza?
CHANZO: FAHARI YETU

Comments