Featured Post

HII NDIYO HALI HALISI YA UCHUMI TANZANIA KWA MWAKA 2017/18

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akitoa maelekezo kwa Benki nchini kuangalia namna ya kupunguza riba kwa wakopaji na pia kufuata vigezo stahiki kwa mkopaji ili kuondoa mikopo chechefu wakati wa mkutano kati yake na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Susana Mkapa na Afisa Mwandamizi wa Wizara hiyo Bw. John Sausi wakizungumza jambo wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na Waandishi wa Habari kuhusu Hali ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/18 katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Maafisa Waandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakifurahia jambo wakati Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo aliangazia suala la hali ya Uchumi na kubainisha kuwa ni imara ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaabani (kushoto) akizungumza na wadau waliohudhuria Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam kulia.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Hali ya  uchumi na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/18 ambapo alitoa agizo kwa vyombo vya ulinzi kuwakamata wanaowalazimisha watanzania kufanya malipo kwa Dola badala ya Shilingi, mkutano ulifanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (mbele) akiwa katika Mkutano na waandishi wa habari kuhusu hali ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/18 katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

Comments