Featured Post

DIWANI KATA YA LASIBULA LINDI AONGOZA WANANCHI UJENZI WA SEKONDARI KWA KUJITOLEA

DIWANI KATA YA LASIBULA LINDI AONGOZA WANANCHI UJENZI WA SEKONDARI KWAKUJITOLEA.


Na Geofrey Jacka-Lindi
Diwani wa kata ya Lasibula Mh.Abdallah Kikwei akishiriki katika ujenzi wa shule ya sekondari ambayo inajengwa na wananchi kwakujitolea.Diwani Kata ya Lasibula mkoani Lindi Mh.Abdallah Kikwei, anaongoza wananchi wa Kata yake katika ujenzi wa shule ya Sekondari kwakujitolea.

Akizungumza na kituochahabari.blogspot.com Kikwei amesema, Wazo la ujenzi wa shule hiyo walikuwa nalo na walishatenga eneo la hekari 25 kwa matumizi ya jamii hivyo wamekata hekari 15 kwaajili ya ujenzi wa shule.
"Tulianza vikao mwezi wa tatu mwaka huu 2017 ili kujadili namna tutakavyoanza ujenzi, na baada ya makubaliano yetu ya kikao tukaazimia tuanze ujenzi mwezi wa tisa, na kweli ujenzi ukaanza"  Alisema Kikwei.
Akizungumzia malengo yao waliyojiwekea Mh. Diwani amesema, wameanza na vyumba sita vya madarasa, huku Mbunge akiahidi kujenga darasa moja na wanatarajia mpaka kufika mwezi wa pili 2018 shule hiyo iwe imefunguliwa ili watoto waliofaulu nakukosa shule waanze kusoma shuleni hapo.
"Tunao wanafunzi 250 waliofaulu lakini wamekosa shule, hivyo hii itakuwa ndio mkombozi wao, wapo watoto waliofaulu kutoka Shule ya msingi Stadium, Lahaleo, Likotwa,Mitwero, Kikwetu na Likong'o"
Baada ya kuona juhudi za Diwani na wananchi Halmashauri wameahidi kusaidia ujenzi huo huku Afisa elimu wa Manispaa amejitolea Bati, Madirisha na Mbao kwaajili ya kupaua, kitendo ambacho kimewapa nguvu zaidi wananchi.
Kata ya Lasibula inajumla ya mitaa kumi ambapo Diwani ameigawanya ili kata tano zijenge Shule na kata tano nyingine zijenge Zahanati ambayo kwasasa wanakusanya michango kama maandalizi ya ujenzi wa Zahanati.


Comments