Featured Post

NMB YAWAFUNDA WAFANYABIASHARA 6200 MIKOA YOTE

 
Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa NMB – Jos Van Lange akitoa mada wakati wa mkutano wa wajasiliamali ulioandaliwa na benki ya NMB. Zaidi ya wafanyabiashara 300 wa Mkoa wa Mtwara walihudhuria mkutano huo ambapo pia walipewa mafunzo ya jinsi ya kukuza biashara zao.
 
Mada mbalimbali zikitolewa katika mkutano huo wa wajasiliamali ulioandaliwa na benki ya NMB. Zaidi ya wafanyabiashara 300 wa Mkoa wa Mtwara walihudhuria mkutano huo ambapo pia walipewa mafunzo ya jinsi ya kukuza biashara zao.

Na Mwandishi Wetu
BENKI ya NMB imeendesha mafunzo kwa wajasiliamali zaidi ya 6200 wa Wilaya na Mikoa yote nchini yenye lengo la kuwapa ujuzi wa jinsi ya kukuza biashara zao kwa maendeleo ya kiuchumi nchini.
Wafanyabiashara hao wamekua wakipewa mafunzo yanayohusu bidhaa zinazotolewa na NMB kama jinsi ya kutunza vitabu vya mahesabu, elimu ya masoko na pia elimu ya mlipa kodi na matumizi bora ya mikopo wanayopatiwa na benki ya NMB.
Akizungumza kwenye moja ya mikutano ya wafanyabiashara Mkoani Mtwara ambapo zaidi ya wajasiliamali 300 walihudhuria. Kaimu Mkuu wa kitengo cha biashara za wateja NMB Donatus Richard -alisema kuwa katika kuwajali Wateja wake wadogo na wakati, NMB imekuwa ikiendesha mafunzo ya wajasiliamali nchi nzima ili kuwapa elimu ya jinsi ya kukuza biashara zao.
“kuna wafanyabiashara ambao walianza na mitaji midogo sana, wameanza kwa kukopa shilingi laki 5 tu na kuziwekeza kwenye biashara, kupitia mafunzo haya na pia ushauri tunaowapa, wamekuza mitaji yao na wengine sasa wanakopa mabilioni ya Fedha kutoka NMB.” Alisema Donatus.
Mafunzo hayo ya wajasiliamali yalifanyika kwa klabu za biashara za katika kila Mkoa na Wilaya ambapo Viongozi mbali mbali wa kiserikari na viongozi wa wafanyabiashara wamekua wakihudhuria hafla hizi. Zaidi ya wafanyabiashara 6200 wamepata na kunufaika na mafunzo kutoka NMB.
NMB imefanya mikutano ya business club 31 nchi nzima zenye wanachama zaidi ya 200 ambao wamekuwa wakifaidika na mafunzo mbalimbali kutoka NMB yanayohusu bidhaa zinazotolewa kwao na benki kama jinsi ya kutunza vitabu vya mahesabu, elimu ya masoko na pia elimu ya mlipa kodi.
Lakini pia Zaidi ya wajasiliamali 1000 walipata nafasi ya kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa mikutano hii kwa wajasiliamali wenzao.
Bwana Donatus alisisitiza kwamba lengo kuu la vilabu hivi vya biashara vimeundwa kuhakikisha wafanyabiashara nchini wanakuza mitaji yao, kuajiri watanzania wengi zaidi na pia kuchangia uchumi wa taifa hili kupitia ulipaji kodi.
  
Baadhi ya washiriki wakijiandikisha kwenye mkutano huo wa wajasiliamali. 
Mkutano wa wajasiliamali ulioandaliwa na benki ya NMB ukiendelea.

Aliongeza kuwa ili kuhakikisha benki hiyo inachangia ukuaji wa sekta ya biashara nchini, imeanzisha vilabu vya wafanyabiashara (NMB Business Clubs) ambao ndio walengwa wa vituo vya biashara.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea –Pololet Mgema akiongea kwenye mkutano wa Business Club iliyofanyika mwanzoni mwa wiki Mkoa wa Songea, aliipongeza benki ya NMB kwa kuonyesha shauku ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi kupitia vilabu vya biashara ambavyo vinawapa wananachi elimu ya kijasiriamali na hivyo kupiga hatua ya kuiuchumi kimaisha.
Mhe. Mgema aliwasihi wafanyabiashara wote nchini kua na nidhamu ya Mikopo kwani wengi wao hupotoka mara wapatapo mitaji ya bishara zao huku wakidhani kuwa pesa itabakia katika mikono yao siku zote.
“Lengo la kuanzisha NMB Business Club ni kuhakikisha wafanyabiashara hawa wanakuza mitaji yao, kuajiri watanzania wengi zaidi na pia kuchangia uchumi wa taifa hili kupitia ulipaji kodi.” Alisema Mgema.
Wafanyabiashara wadogo na wakati wanawakilisha asilimia 14 ya biashara ya NMB.
NMB imeanza kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kuwa wanachama wake wanafikia idadi ya 25,000 kufikia mwishoni mwa mwaka 2017. Wanachama wa klabu ya Biashara (NMB Business club) ni wajasilia mali ambao wamekuwa wakiwezeshwa mara kwa mara na benki kwaajili ya kuendeleza biashara zao.
Nje ya mafunzo na vituo hivi sita vya wafanyabiashara, Wajasiriamali hawa wanapata faida ya kutumia mtandao mpana zaidi wa matawi zaidi ya 200 ya NMB na ATM zaidi ya 700 nchi nzima.

Comments