Featured Post

MHANDISI METHEW MTIGUMWE AZITAKA TAASISI ZA UTAFITI NCHINI KUWANUFAISHA WAKULIMA KUPITIA TAFITI ZAO


Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akikagua baadhi ya vitendeakazi mara baada ya kutembelea Maabara ya Uchambuzi wa Viuatilifu katika Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika ukanda wa Tropiki (TPRI) kilichopo Mkoani Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akikagua baadhi ya mbegu za maharage zilizogunduliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Selian Kanda ya Kaskazini (NZARDI) mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akizungumza na watumishi katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Selian Kanda ya Kaskazini (NZARDI) wakati wa kikao cha kazi.
Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Maendeleo Wizara ya Kilimo Dkt. Hussein Mansoor akielezea jambo mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe mara baada ya kutembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Selian Kanda ya Kaskazini (NZARDI) mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Selian Kanda ya Kaskazini (NZARDI) Dkt Margaret J. Mollel kukagua maabara ya uchambuzi wa Viuatilifu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akikagua baadhi ya mbegu za maharage zilizogunduliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Selian Kanda ya Kaskazini (NZARDI) mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi.
Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Maendeleo Wizara ya Kilimo Dkt. Hussein Mansoor akielezea jambo wakati wa kikao cha kazi na Watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Selian Kanda ya Kaskazini (NZARDI) mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi.
Ukaguzi wa vifaa kazi katika sekta ya kilimo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akipata maelezo ya ufanyaji kazi mara baada ya kutembelea Maabara ya Uchambuzi wa Viuatilifu katika Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika ukanda wa Tropiki (TPRI) kilichopo Mkoani Arusha.


Na Mathias Canal, Arusha

Taasisi za utafiti katika sekta ya kilimo zimetakiwa kuongeza ufanisi katika utaalamu wao ili kuwanufaisha wakulima kote nchini kwani kwa sasa Benki ya Tafiti zilizopo hazijatumika ipasavyo.

Wataalamu wa utafiti wamepaswa kufanya vizuri pia katika eneo la kutangaza tafiti  ikiwemo Kuongeza ujuzi katika Utafiti wa mazao mbalimbali wasiishie katika zao moja au mawili tu.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe alipotembelea Taasisi ya Utafiti ya viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika ukanda wa Tropiki iliyoanzishwa mwaka 1945 yenye jukumu la kuendeleza utafiti na kutoa huduma za matumizi sahihi na salama ya viuatilifu, Taasisi ya utafiti na Mafunzo ya Tengeru, HORTI Tengeru iliyoanzishwa mwaka 1980 sambamba na Kituo cha Utafiti wa kilimo na Maendeleo Selian (SARI) kilichofunguliwa mwaka 1979 kama shamba la utafiti wa ngano na Shayiri chini ya ufadhili wa Canada.

Mhandisi Mtugumwe aliwasihi watafiti hao Kuendelea kufanya juhudi kubwa kuandika miradi mbalimbali kwa ajili ya kusaidia shughuli za uendelezaji wa utafiti kwani bajeti ya serikali pekee haiwezi kutosha.

Alisema wataalamu hao wanapaswa kufanya tafiti kwa kuendana na matakwa ya sekta ya kilimo na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Alisema Wizara ya kilimo ipo tayari kuwakaribisha baadhi ya watafiti kwenye kamati ya Bunge inayoshughulikia kilimo ili kuwasilisha vitu walivyovifanya katika Utafiti mbele ya wabunge ambaomoja ya jukumu lao kubwa ni kutunga sheria.

Kuhusu changamoto za nyumba za wafanyakazi alisema kuwa tayari zipo katika Taasisi na vyuo vyote vya Utafiti hivyo itakapofanywa tathmini yote kwa ajili ya vyuo vya kilimo nchini litatekelezwa pia katika chuo hicho.

Mhandisi Mtigumwe alisema watafiti hao wanapaswaKuwa na mikakati ya kupata vijana wengi zaidi ili waweze kujifunza fani hiyo kuhusu Utafiti kwani bado serikali inatambua kuwa vijana ndio nguvu kazi ya Taifa.

Kuhusu mpango wa Wizara ya Kilimo kwenye Mazao ya mboga mboga na matunda alisema kuwa ni sehemu ya kipaumbele cha Wizara na serikali.

Katika hatua nyingine alisema atawasaidia kutengeneza kitalu nyumba (Green House) kimoja kwa ajili ya kujifunzia

Comments