Featured Post

HII NI ORODHA MPYA YA WALIOPEWA MIKOPO KATIKA AWAMU YA TATU 2017/2018

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetoa orodha ya Awamu ya Tatu ya wanafunzi 7,901 wa Mwaka wa Kwanza waliofanikiwa kupata mikopo na hivyo kufanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo hadi sasa kufikia 29,578.


Katika Awamu ya Kwanza, wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza walipangiwa mikopo na Awamu ya Pili wanafunzi 11,481.

Kiasi cha shilingi 427.54 bilioni zimetengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka 2017/2018 na tayari Serikali imeshatoa shilingi 147.06 bilioni kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka huu wa 2017/2018.


Comments