Featured Post

SABA WANUSUFIKA KIFO WAWILI WAJERUHIWA BAADA YA CARRY WALIYOPANDA KUGONGA TRENI JIJINI TANGA

 Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga wakishuhudia ajali hiyo leo iliyotokea eneo la Kwaminchi makutano ya reli baada ya gari ndogo aina ya Carry kufeli breki baada ya kufika eneo la reli na kuligonga treni iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni Jijini Tanga.
 Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga wakishuhudia ajali hiyo leo iliyotokea eneo la Kwaminchi makutano ya reli baada ya gari ndogo aina ya Carry kufeli breki baada ya kufika eneo la reli na kuligonga treni iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni Jijini Tanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba akikagua gari hiyo jana jioni.
Watu saba wamenusufika kifo huku wawili  wakijeruhiwa vibaya na kupelekwa hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo baada ya gari ndogo waliokuwa wamepanda aina ya Carry kugonga treni ya mizigo iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni ya Tanga.

Kwa mujibu wa mashuhuda walieleza kuwa gari hilo baada ya kufika eneo la makutano ya reli wakati lijaribu kusimama ndipo lilipofeli breki na kuiparamia treni hiyo.

Ajali hiyo ambayo ilitokea jana eneo la makutano ya reli Kwaminchi Jijini  Tanga iliacha mshangao mkubwa kutokana na mazingira ya namna ilivyotoke ambapo gari ndogo ilikuwa ikitokea eneo la kwaminchi.

Akithibitisha kutokea tukio hilo jana,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba alisema ajali hiyo ilitokea saa kumi jioni katika eneo hilo ambapo gari hilo ilifeli breki na kuparamia mabehewa ya reli wakati ikipita katika eneo hilo.

Aliitaja gari hiyo aina ya Carry ambayo ilipata ajali hiyo kuwa ni T.343 DCQ  iliacha njia na kuigonga treli iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuingia  kwenye stesheni ya Tanga.

Aidha alisema majeruhi sana waliokuwepo kwenye ajali hiyo walifikishwa  kwenye hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo kwa matibabu zaidi huku Dereva wa gari hilo alitokomea kusikojulikana.

Kamanda huyo alisema kutokana na kukimbia kwa dereva huyo wataendelea kumsaka ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili.

Hata hivyo,Kamanda huyo alitoa wito kwa madereva kuhakikisha wanazingatia sheria za usalama barabarani kwa kuhakikisha kwenye maeneo ya kivuko cha reli wanakaa mita 50.

Awali akizungumza mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo,Said Kiruwasha alisema wakati wakiwa kwenye eneo hilo wakailiona gari hilo moshi likitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni ndipo gari hilo lilipokuwa likipita ndipo ilipofeli breki baada ya kusikia honi ya treni hiyo.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Comments