Featured Post

MAGONJWA YA SUNGURA: MAAMBUKIZI YA BAKTERIA AU UVIMBE KWENYE TEZI ZA MAZIWA (SEPTIC MASTITIS)


Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini Blog

Septic mastitis ni maambukizi katika tezi za maziwa, tezi ambazo zinatunga maziwa baada ya mnyama kuzaa.
Maambukizi haya hutokea wakati kunapokuwepo na ongezeko la bacteria katika tezi za maziwa.

Kama tatizo hili litaachwa bila kutibiwa, bacteria wanaweza kusambaa hadi kwenye damu na kwenye tezi za limfu, na kuathiri mwili mzima na kuhatarisha maisha ya mnyama.
Kama maambukizi hayo yatabakia kwenye tezi za maziwa (mammary glands), usaha (abscess) unaweza kuonekana kwenye tezi hizo.
Uvimbe wa matiti (cystic mastitis), ambao unatokana na maji yaliyojaa kwenye uvimbe, au vifuko vya maji maji vilivyochukua nafasi ndani ya tishu za mwili, pia vinaweza kutokea kwenye tezi na mirija ya tezi za maziwa (ambazo ni sawa na matiti ya binadamu).
Uvimbe huo huwa umejaa maji ya utasa au ugumba. Hali hii pia inasababishwa na uvimbe mwingine kama huo kwenye mji wa uzazi na vifuko vya mayai ya uzazi.
Kama hautatibiwa, uvimbe wa matiti unaweza kusababisha saratani. Mara nyingi wanaoathirika zaidi ni sungura wenye umri wa kuzaa ama wanyonyeshao.

Dalili na Aina

Uvimbe wa tezi za maziwa
* Kukosa hamu ya kula (Anorexia), uchovu, kukosa nguvu, kupungua uzito (lethargy), mfadhaiko
* Kupata kiu kubwa na kukojoa sana (polydipsia, polyuria)
* Dalili za mimba bandia (kama vile, kujinyonyoa manyoya, kujenga kiota cha kujifungulia, mimba ya uongo)
* Kugua au kifo kwa watoto.

Uvimbe wa matiti
* Mara nyingi mjanja, yuko makini sana, hana maumivu
* Damu katika mkojo (hematuria), ambayo mara nyingi inahusisha magonjwa kwenye mji wa uzazi
* Homan a kupungukiwa maji.

Uchunguzi

Uchunguzi wa kawaida wa nje unaweza kuonyesha uvimbe mbichi, mgumu, ulioiva, na tezi nyekundu za maziwa, na kuonekana kwa majimaji kwenye matiti (ambayo siyo maziwa) kutoka kwenye tezi za matiti au chuchu.
Anaweza pia kuwa na homa kali pamoja na uchovu.
Uchunguzi wa kina wa damu unapaswa kufanyika, pamoja na uchunguzi wa damu wa kikemia, kujua kiasi cha wingi wa damu, na kupima mkojo (urinalysis).
Vipimo hivi ndivyo vinavyoweza kubaini kama kuna maambukizi yoyote.

Tiba

Kama maambukizi ni makubwa, ya kudumu, au yanajirudia, ni vyema upasuaji ufanyike kuondoa tezi za matiti na vifuko vya mayai na mji wa uzazi kwa afya ya sungura wako.
Kama maambukizi yatawahiwa mapema, na hayataonekana kuwa katika kiwango kikubwa, dawa za maumivu za aina ya antibiotics ambazo ni maalum kwa ajili ya bacteria waliomo zinaweza kutolewa kwa uangalifu mno.

Maisha na Matunzo

Unapaswa kudumisha mazingira wanamoishi sungura wako ili kuzuia maambukizi mapya.
Kama sungura wako wamebainika kuwa na uvimbe wa tezi za uzazi, na hali inajirudia ama ni ya kudumu, inashauriwa kuondoa tezi za matiti kwa sababu uvimbe huo unaweza kuendelea na kuzaa kansa.

Imeandaliwa na www.maendeleovijijini.blogspot.com. Tupigie: +255 656 331974


Comments