Featured Post

MAGONJWA YA SUNGURA: DALILI NA SABABU ZA SUNGURA KUPATA KANSA YA KIZAZI (UTERINE ADENOCARCINOMA)


Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini Blog

UVIMBE wa uterine adenocarcinoma, unaofanana na tezi kama uvimbe wa malignant unaotokana na tishu za ndani kutoka katika eneo la ndani kabisa la mji wa uzazi, ni miongoni mwa visababishi vya kansa ya kizazi kwa sungura.
Takriban asilimia 60 ya sungura majike wenye umri wa zaidi ya miaka mitatu wanaweza kupatwa na tatizo hili.

Uvimbe huu mara nyingi hutokea katika eneo la ndani la mji wa uzazi au katika ukingo wa mji wa uzazi.
Mara nyingi kansa ya kizazi hutokea baada ya sungura kupata matatizo mengine ya uzazi kwenye kizazi, ikiwemo kitu kinachoitwa endometriosis, hali ya maumivu yanayohusisha kukua kwa tishu kwenye uterus na via vya uzazi.
Umri unaonekana kuwa chanzo kikuu cha tatizo hili.
Uvimbe unaweza kuonekana pia pamoja na hali nyingine, kama kuvimba kwa mishipa ya vena katika ukingo wa mji wa uzazi, hali ambayo pia kitaalam huitwa venous aneurysms.

Dalili na Aina

Dalili na viashiria vya kansa ya kizazi (uterine adenocarcinoma) inatofautia kutoka kwa sungura mmoja hadi mwingine, japokuwa sungura yeyote jike mwenye zaidi ya miaka 3-4 anaweza kupata.
Kuonekana kwa damu katika mkojo kunaweza kuwa dalili kubwa kwa sungura majike, lakini dalili nyingine ni pamoja na:
* Kutoka majimaji kwenye uke yaliyochanganyika na damu
* Uvimbe kwenye tezi za maziwa, na majimaji meupe yanayoweza kutoka kwenye matiti (lakini siyo maziwa)
* Kubadilika kwa tabia, ikiwemo tahayari
* Uchovu na kukosa nguvu, kushindwa kula, utando mweupe (hasa katika hatua za mwisho za ugonjwa)
* Tungamo (mass) katika utumbo (hutokea katika hatua za mwisho za ugonjwa)
* Kukua kwa matiti.

Chanzo 

Sungura yeyote jike ambaye bado anaendelea kuzaa anaweza kupata kansa ya kizazi.

Uchunguzi

Uchunguzi mara nyingi huanza kwa kuzitenga sababu nyingine za dalili kama hizo, ikiwemo chanzo kikubwa cha kuwepo kwa tungamo kwenye tumbo: yaani mimba.
Uvimbe mwingine usio wa kizazi unaweza kusababisha dalili kama zilizoelezwa hapo juu.
Kukua sana kwa seli kunaweza pia kuendana na dalili nyingine za uvimbe; hata hivyo, dalili ambazo zimeelezwa hapa zinatajwa kwamba ni za uwepo wa kansa, hasa kwa sungura wenye zaidi ya umri wa miaka mitatu.
Upungufu mkubwa wa damu (Anemia) mara nyingi unaendana na hali hii kwa sungura majike na unasaidia katika kufanya uchunguzi.
Picha mbaya katika vipimo vya maumbo kama X-Ray na Ultrasound pia vinaweza kusaidia kubaini tatizo, kama ilivyo kwa uvimbe usio wa kawaida au limfu, ambao unaashiria kusambaa kwa ugonjwa.
Uchunguzi pia unaweza kufanya kwa kutumia matokeo ya biopsy kwenye tishu ya kizazi.

Tiba

Tiba ya kansa ya kizazi (uterine adenocarcinoma) inaweza kuhusisha kuondolewa kwa viungo ambavyo tayari vimeathirika na kansa (complete hysterectomy).
Kwa kawaida hii ni hatua ya awali, hususan kama kansa haijasambaa hadi kwenye via vya uzazi.
Uchunguzi wa biopsy unaweza kufanyika kuthibitisha mabaki ya kansa kwenye via vya uzazi, au kama imeenea nje ya via vya uzazi.
Wakati mwingine hakuna dalili za kuenea kwa kansa wakati wa kufanya upasuaji.
Ufuatiliaji ni muhimu sana wakati wa tiba hasa kwa kupunguza maumivu kwa sungura.

Imeandaliwa na www.maendeleovijijini.blogspot.com. Tupigie: +255 656 331974


Comments