Featured Post

IGP SIRRO ATUA RUVUMA, AZUNGUMZA NA WANANCHI KUTII SHERIA BILA SHURUTI

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na wananchi wa eneo la Lizaboni wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, na kuwataka kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo na kutii sheria za nchi pamoja na kuwafichua wahalifu waliopo kwenye jamii, IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Picha na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akimsikiliza Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma (SACP) Gemini Mushy, alipowasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzungumza na maofisa na askari kuona changamoto zao ikiwa pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki na kutoa huduma bora kwa wananchi. Picha na Jeshi la Polisi.
Askari wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu na wahalifu katika mkoa wa Ruvuma, wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, na kuwataka kufanyakazi kwa kuzingatia sheria na taratibu pamoja na kutimiza wajibu wao wa kutenda haki wanapotekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro (watatu kulia kwenye meza kuu) na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Binilith Mahenge,  wakiwa kwenye kikao cha pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo, IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzungumza na Maofisa na askari na kuona changamoto zao ikiwa pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki na kutoa huduma bora kwa wananchi. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akiwasalimia wanafunzi wanaosoma shule ya msingi Wilayani Songea, aliokutananao uwanja wa ndege mkoa wa Ruvuma, muda mfupi baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzungumza na Maofisa na askari na kuona changamoto zao ikiwa pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki na kutoa huduma bora kwa wananchi. Picha na Jeshi la Polisi.

Comments