Featured Post

CHAMBAVU (BLACK QUARTER) UGONJWA UNAOSAMBAZWA KUPITIA KWENYE UDONGO

Ng'ombe anayeumwa Chambavu akiwa amelala. Picha ndogo inaonyesha kidonda kikubwa kwenye mguu kilichotokana na ugonjwa huo.

 

UGONJWA wa Chambavu au Black Quarter unaoshambulia ng'ombe, kondoo na mara chache farasi.

Ugonjwa huu unasababishwa na vijidudu aina ya Clostridium chauvoei ambavyo hushambulia bila uwepo wa Oksijeni ya kutosha (anaerobic) na kuzalisha sumu kwenye mwili wa mnyama na kusababisha kifo.

KUSAMBAA
Vijidudu vya Clostridium chauvoei husambaa kwa kupitia kwenye udongo ambapo mnyama huvipata anapokula majani.
Lakini pia ugonjwa huu huweza kusambazwa kwa njia ya vidonda na mate kutoka kwa mnyama mwenye ugonjwa huu.

DALILI
-Homa kali
-Misuli ya miguu ya nyuma huvimba na kuwa na joto kali, inauma ikiguswa na rangi ya sehemu hiyo ya ngozi hubadilika
-Ukigusa sehemu iliyoshambuliwa inatoa sauti kama ya majani makavu
-Mnyama huchechemea mguu wa nyuma sababu ya maumivu.

UCHUNGUZI
Nyama ya ng'ombe aliyekufa kwa ugonjwa wa Chambavu ikifanyiwa uchunguzi.

Uchunguzi ufanyike na maofisa ugani wa mifugo kwa kufuatilia dalili na historia ya sehemu husika
-Kipande cha msuli na majimaji kutoka sehemu iliyoathiriwa kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara
-Uchunguzi wa mwili wa mnyama aliyekufa (Post Mortem).

MATIBABU
-Tumia dawa za aina ya Penicilin ambazo zinasaidia kutibu ugonjwa kama matibabu yataanza katika hatua za mwazo, ukichelewa hutaweza kumtibu mnyama wako.
-Tumia B-Complex na dawa za kupunguza uvimbe kama visaidizi vya tiba
-Chana sehemu iliyoathirika ili kutoa majimaji na kuingiza hewa ili kuharibu mazingira ya vijidudu hivyo kuishi.

KINGA
-Chanjo ya mara moja kwa mwaka kwa wanyama wakubwa.
-Wanyama wadogo wachanjwe mara wafikishapo umri wa miezi mitatu
-Kwa sehemu ambayo kuna mlipuko wa ugonjwa huu wanyama wote wachanjwe kisha wapigwe dozi kubwa ya penicilin (kama ugonjwa hautaibuka ndani ya siku 14 wanyama wako watakuwa salama)
-Miili ya wanyama waliokufa ichomwe moto na kuzikwa kwenye shimo refu sana ili kuondoa uwezekano wa vijidudu hivyo kusambaa.



Comments