Featured Post

MWAKYEMBE AWAONGOZA WANAHABARI KUUAGA MWILI WA MUHINGO RWEYEMAMU DAR


 Roseline Rweyemamu (katikati) ambaye ni Mjane wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni na Mwanahabari Mkongwe, Muhingo Rweyemamu, akiweka shada la Ua juu ya Kaburi la mumewe wakati maziko katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam jioni hii.

 Watoto wa Marehemu, Muhingo Rweyemamu ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni na Mwanahabari Mkongwe wakati wa maziko yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA NA VENANCE NESTORY
 Wakuu wa Wilaya Wastaafu, wakiweka Shada la Ua juu ya Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni na Mwanahabari Mkongwe, Muhingo Rweyemamu wakati wa maziko katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam
 Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu (wa pili kushoto), akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo na Burudani (TASWA0, Juma Pinto wakati wa shughuli ya kumuaga mwanahabari mkongwe,marehemu  Muhingo Rweyemamu. Kulia ni Benny Kisaka na kushoto ni Mwandishi wa habari za Michezo wa Gazeti la Jambo Leo, Asha Kigundula
 Sehemu ya waombolezaji wakisubiri kuaga mwili wa  marehemu Rweyemamu
 Wanahabari wakirekodi tukio hilo

 Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Mtanzania, ambaye pia alikuwa rafiki mkubwa wa marehemu Muhingo, akitoa salamu za rambirambi
 Mtoto wa marehemu Muhingo, Emmanuel  akisoma wasifu wa marehemu babake
 Wajumbe wa kamati ya mazishi ya marehemu, Muhingo, wakijadiliana jambo wakati wa kuuaga mwili. Kutoka kushoto ni Joyce Mmasi, Mgaya Kingoba, Theiphil Makunga, Abubakar Liongo na Benjamin Thomson
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk, Harrison Mwakyembe akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Muhingo kwenye viwanja vya Mnazi mmoja Dar es Salaam
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Muhingo
 Sophia Mjema akimfariji mjane wa Muhingo, Roseline
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe akimfariji mjane wa marehemu Muhingo, Rweyemamu
 Waombolezaji wakipita kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu,Muhingo
 Mpigapicha wa zamani wa Daily News, Athuman Khamisi akimfariji mjane wa marehemu, Roseline
 Baadhi ya wanahabari wakitoa heshima za mwisho, mbele ni Nyaronyo Kicheere
 Wanahabari wakitoa heshima za mwisho

 Mama mkwe wa marehemu, Muhingo, akilia baada ya kutoa heshima za mwisho
 Roseline Rweyemamu (katikati) ambaye ni Mjane wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni na Mwanahabari Mkongwe, akiugusa mwili wa mumewe wakati wa kuaga.
Waandishi wa habari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari Mkongwe, Muhingo Rweyemamu baada ya kuutolea heshima za mwisho kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam

Comments