Featured Post

BANGI ILIVYOPAISHA UCHUMI WA JIMBO LA COLORADO NCHINI MAREKANI


New York, Marekani
KAMA ingekuwa ni Tanzania, ukifika dukani ungeuliwa: "Unataka cha Arusha, Makambako, Morogoro au Malawi?" Lakini sasa huko ni Marekani, taifa kubwa linaloongoza kwa uchumi duniani.
Na Jimbo la Colorado nchini humo ndilo lenye uchumi unaokua kwa kasi zaidi kuliko majimbo mengine yote 51 yaliyobakia.
Ukuaji huo unatokana na kitendo cha Serikali ya jimbo hilo kuhalalisha matumuizi ya bangi na mimea kama hiyo Januari 2012.

Kwa sasa jimboni humo maduka ya kuuza bangi na mimea kama mhiyo yanaingiza jumla ya dolari milioni 295 (sawa na shilingi bilioni 590 za Tanzania) huku Derikali ikipata jumla ya Dola 51 milioni (sawa na Shs. 112.2 bilioni za Tanzania) kama kodi ya mapato.
Taarifa zinasema kuwa kutokana na hatua hiyo ya Serikali ya kuruhusu matumizi ya bangi, utalii jimboni humo umeongezeka maradufu huku vituo vya afya vya tiba kwa wanaopata madhara vikiongezeka pia.
Hata hivyo, pamoja na kwamba bangi ni halali jimboni Colorado, lakini inauzwa kwa watu wenye umri kuanzia miaka 21 na kuendelea na si chini ya umri huo.
Uangalizi makini hufanywa kwenye maduka yanayouza bangi hiyo na yeyote anayekwenda kinyume cha amri hiyo hujikuta akifikishwa mbele ya sheria na vyombo vya dola.
Inaelezwa kwamba watu wengi wanapenda kutumia bangi kutokana na kwamba huwasaidia kupunguza maumivu ya mwili na uchovu wa usingizi.
Ziko bidhaa nyingine ambazo huwekwa unga wenye bangi kama vile mananasi, maembe, nyanya na vitu vingine vya majimaji au mafuta ambavyo watu hupenda kutumia na hivyo kujikuta wakiliongezea jimbo hilo pato la ajabu na kuongoza kwa uchumi nchini Marekani.
Rais wa zamani wa Marekani, Barak Obama, katika kampeni zake za kuwania Urais wa nchi hiyo mwaka 2008, alikiri kuwa amewahi kuvuta bangi na kusema kuwa ni bora kuliko sigara.

Hata hivyo, bangi imepigwa marufu sehemu nyingi duniani ikiwemo Tanzania kwa madai kuwa inahatarisha maisha ya watu.


Comments