Featured Post

AVUNJWA MGUU KWA RISASI

Mkazi wa kitongoji cha Endevesi, Kata ya Oljoro wilaya ya Arumeru,Hwanga Ndaskoy(30)amefunjika mkuu wake wa kulia baada ya watu wanaodaiwa kuwa ni askari polisi mkoani Arusha, wapatao nane kumvamia na kumpigwa risasi ,akiwa shambani kwake.

Akizungumza kwa masikitiko nyumbani kwake, baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya Mount Meru alikokuwa amelazwa kwa zaidi ya wiki moja,Ndaskoy ameeleza kwamba tukio hilo limetokea mnamo,Agost 31,mwaka huu majira ya saa saba wakati akivuna mahindi shambani kwake akiwa na familia yake.
Alisema kua alifuatwa na askari hao waliokuwa wamevalia kiraia na mmoja  mwenye silaha akiwa amevaa sare za kipolisi.
Pia askari hao walikuwa wameongozana na mkazi mmoja wa kitongoji hicho aliyemtaja kwa jina la ,Yohane Palay aliyemtambua kuwa ni baba mkwe wake .

‘’Nilimsikia baba mkwe akiwaelekeza askari hao wanikamate huku akiwatahadhalisha kuwa mimi ni mkorofi na wasinisogelee nitawakata na sime jambo ambalo sio kweli,ndipo askari mmoja mwenye silaha aliponifyatulia risasi  ya mguu na kuanguka chini’’alisema Ndaskoy
Aidha alisema askari baada kumpiga risasi walimpakia kwenye gari lao na kumpeleka katika hospital ya Mkoa Mt,Meru ambapo walimweleza daktari kuwa ameanguka na pikipili Jambo ambalo si kweli.

Alieleza kuwa kabla ya tukio hilo ,Agost 26 mwaka huu ,aligombana na mke wa kaka yake aitwaye ,Jehova Baraka ambaye wanaishi jirani baada ya mbuzi kula mahindi yake yaliyokuwa nyumbani .

Alisema ugomvi huo ulienda mbali zaidi kiasi cha kutoleana maneno makali ,ambapo Jehova aliamua kwenda kwa baba yake mzazi aitwaye Yohane Palay na kutoa taarifa kuwa amepigwa na shemeji yake .

Palay aliamua kwenda kituo cha polisi cha Mbauda jijini hapa na kutoa taarifa juu ya tukio hilo,hata hivyo viongozi wa kitongoji hicho wakiwemo wazee wa ukoo waliingilia kati na kumtaka Palay alirejeshe nyumbani ili wazee wa ukoo walipatie ufumbuzi wa kudumu jambo ambalo waliafikiana.

Alisema Kikao cha ukoo kiliketi,agost 30 na kukubaliana kumaliza jambo hilo kwa kuwatoza faini za kimila wahusika wote wawili baada ya kubaini wote wanamakosa,hata hivyo walishangaa kesho yake agost 31 kufuatwa na polisi na kupigwa risasi.

Kwa upande wake,Palay alikiri kupeleka malalamiko yake kituo cha polisi ,Mbauda ,akidai kuwa mtoto wake,ambaye ni mke wa kaka yake na majeruhi alipigwa na kudhalilishwa. Hata hivyo aalikana kuwarubuni Polisi ili wampige risasi mtuhumiwa

Akizungumzia tukio hilo,kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo alisema kuwa anafuatilia undani wa tukio hilo ikiwemo kubaini ni askari gani walienda kwenye tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi.

"Kwa kweli sina taarifa ya tukio kama hilo ila nitachunguza  kama lipo nitalitolea ufafanuzi" Kauli ya Mkumbo.

Mkumbo alisema analifanyia  uchunguzi jambo hilo kupitia wasaidizi wake na kuahidi kuchukua hatua kali iwapo itabainika hapakuwa na ulazima wa matumizi makubwa ya silaha ya moto kwa askari wake.
Na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini blog 

Comments