- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya akina mama waliofika kupata huduma kwenye kituo hicho cha afya.
Ofisa Muuguzi Msaidizi Darous
Bakari akisoma taarifa ya kituo cha afya cha Matai Wilayni Kalambo wakati wa
mkutano wa Waziri wa Afya alipokuwa akizungumza na watumishi wa kituo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya ya Kalambo
Julieth Binyuru akisalimiana na akina mama hao waliokuwa wakisubiri kuwajulia
hali wagonjwa wao waliolazwa kwenye kituo vha afya cha Matai.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto akimjulia hali mama aliyejifungua kwenye wodi ya
wazazi kituoni hapo.
Baadhi ya Watumishi wa Kituo cha
afya cha Matai wakimsikiliza Waziri huyo wakati aluipofanya ziara kwenye kituo
cha afya kwa ajili ya kujione hali ya utoaji huduma za afya Mkoani Rukwa.
Msafara huo wakiangalia jengo la
maabara(halipo pichani) wakati wa ukaguzi wa majengo yaliyopo kituo cha afya
Matai Kushoto ni waziri Ummy Mwalimu,katikati ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Dkt.Boniface Kasulu na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Julieth
Binyura(Picha zote na Wizara ya Afya)
Na WAMJW-Kalambo
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amewataka
watoa huduma za afya katika kituo cha
afya cha Matei wilayani Kalambo kutoa huduma bora kwa wanawake wajawazito
Rai
hiyo imetolewa jana na Waziri huyo alipokuwa kwenye ziara ya kikazi wilayani
hapo na kutembelea hospitali hiyo pamoja na kuongea na watumishi wa sekta ya
afya kujua changamoto zinazowakabili
Alisema
wajawazito wanapaswa kupata huduma bora kila wanapofika kliniki kila mwezi kwa
kuangaliwa mfano dalili za kifafa cha mimba ,wigi wa proteini pamoja na
viatarishi vingine vinavyoweza
kusababisha uzazi pingamizi na hivyo
kupelekea vifo kwa mama au mtoto wakatiwa kujifungua
“Nawapongeza
sana kwa kutenga dirisha la wazee ila kusiwepo tu dirisha bali muwape dawa
wazee wasio kuwa na uwezo,hivyo kama kuwakatia mfuko wa bima ya jamii (CHF)ni
gharama basi wapatieni vitambulisho vya matibabu bure ili wazee wakija kwenye
matibabu wasije na barua za watendaji wa vijiji”
Kwa
upande wa madawa Waziri Ummy amewaambia watendaji hao hakuna masharti magumu ya
ununuzi wa madawa na vifaa tiba kwa kutumia pesa za CHF“nimeshawaambia MSD
ndani ya masaa ishirini na nne umeagiza vitu MSD hana,ndani ya masaa hayo kama
hana unaruhusiwa kwenda kununua unapotaka kwenda”hivyo ni vyema wakapitisha
wadhaburi watakaokuwa wananunua.
“Tangu
serikali hii iingie madarakani imefanya mabadiliko makubwa katika upatikanaji
wa dawa kwa kuongezwa bajeti ya dawa kwa asilimia kubwa,hizi changamoto
ndogondogo zipo ila mwisho wa siku wananchi wanahitaji dawa,hivyo kuhakikisha
dawa zile muhimu zinapatikana wakati wote.
Hata
hivyo amewataka kuwapa kipaumbele wale wanaotumia bima ya afya,nataka kuona
mnaongeza wananchi watakaotumia bima ya afya kwenye matibabu ili kuweza kutatua
changamoto za sekta ya afya
Upande
wa Malaria Waziri Ummy vipimo vya haraka vya malaria vya MRTD ni bure pamoja na
dawa ya kutibu Malaria’ALU’ ni bure”asije kuwaambia mtu kipimo hicho utoe
pesa,sindano kama mtu amezidiwa na maralia kali ni bure”alisisitiza Waziri Ummy
Akiongelea
ugonjwa wa Kifua Kikuu”TB” Waziri huyo alisema ni wakati wa kuwaambiwa watu Tb
inatibika kwani katika kila watu mia moja wanaoumwa kifua kikuu na kutumia dawa
watu tisini wanapona kabisa na wanaendelea na shughuli zao.
Comments
Post a Comment