Featured Post

PROSPER GASPER NA ERICK SIMON NDIO WANAFUNZI MABINGWA WA SAYANSI 2017


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Profesa Simon Msanjila akikabidhi zawadi kwa Prosper Gasper na Erick Simon kutoka Shule ya Sekondari St. Jude's jijini Arusha baada ya kuibuka washindi wa jumla wa Mashindano ya Wanasayansi Chipukizi (YST) yaliyofanyika leo yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Profesa Simon Msanjila akitangaza majina ya washindi wa jumla wa mashindano ya Wanasayansi Chipukizi (YST) yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Royal Dutch Shell Afrika Mashariki  na BG Tanzania Marc Den Hartog akishuhudia.

Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini Blog
PEOSPER Gasper na Erick Simon, wanafunzi wa shule ya sekondari ya St. Jude’s kutoka Arusha, leo wameibuka mabingwa wa jumla wa sayansi katika Maonyesho ya Wanasayansi Chipukizi Tanzania yaliyoandaliwa na Shirika la Wanasayansi Chipukizi Tanzania (Young Scientists Tanzania – YST) ambayo yamefanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi hao ambao walikabidhiwa medali na tuzo na mgeni rasmi, Profesa Simon Msanjila, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, wamewashinda wanafunzi wenzao 198 kutoka shule 100 za mikoa 26 ya Tanzania.
MaendeleoVijijini ilishuhudia wazo lao la “Kutumia Simu za Mkononi kama Mfumo wa Kubaini Ajali za Moto” (The Use of Mobile Network as a Fire Alert System) likiyashinda mawazo mengine 99 yaliyowasilishwa mwaka huu katika maonyesho hayo ambayo yalifanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).
Katika wazo lao hilo, wamebuni mfumo wa kubaini, kwa kutumia simu za mkononi, uwepo wa moto pamoja na wizi kwa kuweka ving’amuzi vinavyoweza kubaini mapema hata kama mtu hayuko nyumbani au akiwa amelala.
MaendeleoVijijini inafahamu kwamba, kumekuwepo na ongezeko kubwa la ushiriki wa shule za sekondari kutoka shule 4 mwaka 2011 hadi 100 mwaka huu, hatua ambayo imetokana na hamasa ya kuendeleza masomo ya sayansi kwa shule mbalimbali za sekondari nchini.
Kwa ushindi huo, mbali ya kutunukiwa medali na tuzo, pia wamepata kitita cha Shs. 1,800,000 pamoja na udhamini wa masomo yao hadi elimu ya juu.
Aidha, wamepata nafasi kwa mara ya kwanza ya kushiriki mashindano ya ubunifu wa sayansi na teknolojia yatakayofanyika jijini Johannesburg, Afrika Kusini mwezi Oktoba mwaka huu na mwakani watashiriki maonyesho ya kimataifa ya sayansi na teknolojia jijini Dublin, Ireland.
Washindi wa pili wa jumla ni kutoka Shule ya Sekondari Kilakala mjini Morogoro.
Maonyesho hayo ambayo ambayo yamedhaminiwa na kampuni ya BG Tanzania ambayo ni mdhamini mkuu, yameshuhudia washindi katika nyanja mbalimbali wakizawadiwa fedha taslimu, vikombe, medali, vifaa vya maabara, vitabu pamoja na udhamini wa masomo ya elimu ya juu (scholarships) katika sayansi katika vyuo vikuu mbalimbali.
Zawadi katika maonyesho hayo ziko katika makundi manne ambayo ni Sayansi ya Baolojia na Ikolojia (Biological and Ecological Sciences) iliyodhaminiwa na Kampuni ya uchimbaji gesi ya Human Development Innovation Fund (HDIF); Sayansi ya Kemia, Hisabati na Fizikia (Chemical, Mathematical and Physical Sciences) iliyodhaminiwa na Kampuni ya Songas; Sayansi ya Kijamii na Kitabia (Social and Behavioural Sciences) iliyodhaminiwa na Shirika la Concern Worldwide; na Teknolojia (Technology) iliyodhaminiwa na Karimjee Jivanjee Foundation.
Aidha, wadhamini wengine wa maonyesho hayo ni Taasisi ya Fizikia (Institute of Physics), Read International, Solaris, Karimjee Jivanjee, First Car Rental, Vernier Software & Technology, Tyndall, na  Statoil kutoka Norway.

Orodha ya washindi wa tuzo maalum mwaka 2017 ambao pamoja na nidhani na tuzo, walipata Shs. 300,000 ni:
Tuzo ya Kupenda Sayansi ya Songas: Clemence Tafiti na Emilian Haule kutoka Kigonsera, Ruvuma na utafiti wao ‘A Simple Electric Circuit As A Security System’.
Tuzo ya Read International: Lucas Kibila na Stide Shedrack kutoka Mmwananchi Sekondari, Kigoma na andiko lao la ‘Is the Bryophyllum Plant a Natural Laboratory Reagent?’. Tuzo hii inahusisha kutoa vitabu vya elimu kwa ajili ya maktaba ya shule.
Tuzo ya First Car Rental: Swaumu Makongoro na Raynarious Zakaria kutoka Shule ya Sekondari Arusha Modern, Arusha na andiko lao la ‘The Dependency of Petroleum in Arusha’.
Tuzo ya HDIF: Abdul Rahman Banisheyba na Hudhaifat Hamdani kutoka Souza Sekondari, Zanzibar na andiko lao la ‘Edible Bug Juice’.
Tuzo ya Taasisi ya Fizikia (IoP): Ester Madoro na Mariam Senge kutoka Kijota Sekondari, Singida na andiko lao la ‘Can Rosella Flowers From Our Environment Solve The Problem of Importing Litmus Papers?’.
Tuzo ya Tyndall/IPIC: Mariam Mwanga na Asila Ibrahim kutoka Mkwakwani Sekondari, Tanga na ubunifu wao wa ‘An Inexpensive Local Solar Water Distillation in School Laboratories’.
Tuzo ya Statoil: Focus Seth na Zuhura Riziki kutoka Macechu Sekondari, Tanga na wazo lao la ‘Kutumia ICT Kutatua Changamoto ya Matokeo ya Wanafunzi wa Bweni wa Shule za Msingi Tanga’ (ICT Solution for Students’ Results Problem in Boarding Primary Schools in Tanga City).
Tuzo ya Maalum Karimjee Jivanjee ya Ufadhili wa Masomo: Stephano Chacha na Naima Mohamed kutoka Vingunguti Sekondari, Dar es Salaam na ubunifu wao wa kutumia mashine ya kilimo inayotumia umeme-jua (Free Energy Farming Tool). Wanafunzi hao walipata Tuzo ya Udhamini (scholarship) wa elimu hadi shahada ya kwanza kutoka taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation.
Tuzo Maalum ya Mwalimu: Mwalimu Hilda Mwaja wa Shule ya Sekondari Nasa mkoani Simiyu ambaye alipata pia kitita cha Shs. 150,000. Tuzo hiyo maalum inatambua mchango wa mwalimu katika kuendeleza sayansi katika mkoa, wanafunzi na shule.

Washindi wa makundi mbalimbali ambao walipata tuzo, nishani pamoja na vitita vya fedha – Shs. 750,000 (mshindi wa kwanza); Shs. 550,000 (mshindi wa pili); na Shs. 350,000 (mshindi wa tatu):
Sayansi ya Baolojia na Ikolojia:
1. Bryson Quambatia na Geoffrey Nasser kutoka Mzumbe Sekondari, Morogoro na utafiti wao wa ‘The Turning Point Towards The Flourishment Of the Agricultural Sector In Tanzania’.
2. Redempotius Respicius na Baris Rajab kutoka Ihundo Sekondari, Kagera na utafiti wao wa ‘Local Way of Detecting Soil pH In Order To Improve Agriculture Sector’.
3. Mapacha Brenda Crispin na Beatrice Crispin kutoka Shule ya Sekondari ya Aquinas ya mkoani Mtwara na andiko lao la Dawa Mbadala ya Mbu kwa Kutumia Mazao na Mimea Asilia’ (An Alternative Mosquito Repellent Using Local Organic Material).

Sayansi ya Kemia, Hisabati na Fizikia:
1. Editha Timothy na Specioza Magesa kutoka Premier Girls, Bagamoyo ambao utafiti wao ulihusu ‘Uchunguzi wa Mionzi Kutambua Metali za Sumu Katika Udongo’ (Use Of Field Portable X-Ray Fluorescence Analyzer to Determined The Content Of Toxic Metals In Soil From Densely Populated Mwambao Bagamoyo And Sinza Dar es Salaam Areas).
2. Justine Justine na Dennis Albin kutoka Bariadi Sekondari, Simiyu na utafiti wao wa ‘Utilizing Plastic Waste’. Ubunifu wao unahusu kuyeyusha bidhaa za plastiki na kuchuja mvuke kuzalisha dizeli na mabaki yake kupata mkaa na Sulfur .
3. Lameck Masau na Nadia Kabwe kutoka Edmund Rice Sinon, Arusha na wazo lao la ‘Simple Hot Shower Invention for Large Groups’ (Mtambo wa kuchemsha maji ya kuoga kwa kutumia mvuko).

Sayansi ya Kijamii na Kitabia:
1. Julius Luchiga na Stanley Paul kutoka Ilongero Sekondari, Singida na utafiti wao wa ‘The Household Hunger Score Project’ (Mradi wa Kupambana na Janga la Njaa).
2. Elizabeth Hange na Salma Mbano wa Shule ya Sekondari Loyola jijini Dar es Salaam na utafiti wao wa ‘Pink Box Project’.
3. Masha Mbwana na Heavenlight Mshomi kutoka Mtwara Girls Sekondari na utafiti wao wa ‘Uhaba wa Walimu wa Sayansi ni Tatizo Sugu Mtwara?’ (Is Science Teacher Shortage a Problem in Mtwara?).

Teknolojia:
1. Francis Shirima na Adolf Katambi kutoka Maua Seminari, Kilimanjaro na utafiti wao wa ‘Educating The Deaf Using Speech Recognition’ (Namna ya kuwafundisha viziwi kwa kutumia utambuzi wa sauti).
2. Khatibu Mgunya na Yasin Bahati kutoka Same Sekondari, Kilimanjaro na utafiti wao wa ‘Automatic Wireless Charger’ (Kifaa cha kuchajia simu kisichotumia waya).
3. Frank Kapinga na Joel Kajiru kutoka Kibaha Sekondari na utafiti wao wa ‘Swichi ya Umeme Inayotumia Sauti’ (Sound Controlled Electric Switch).


Comments