Featured Post

NHIF WATAKIWA KUONGEZA WANACHAMA WASIO WAAJIRIWA

Baadhi ya Watumishi wa Kituo cha afya cha Matai wakimsikiliza Waziri huyo wakati aluipofanya ziara kwenye kituo cha afya kwa ajili ya kujione hali ya utoaji huduma za afya Mkoani Rukwa.

Na WAMJW-Rukwa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wametakiwa kuongeza jitahada za kuwasajili wanachama wengi wa mfuko huo ili vituo vya serikali viweze kutoa huduma kwa wananchi wengi
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipotembelea kituo cha afya cha Mazwi kilichopo katika Manispaa ya Wilaya ya Sumbawanga mwishoni mwa wiki.
Alisema Mkoa wa Rukwa umefikia asilimia 27 ya wananchi wanaotumia bima ya afya Kitaifa,hivyo waongeze kuwashawishi wananchi wengi zaidi kujiunga na mfuko huo pamoja na mfuko wa afya ya jamii(CHF)
“nimesema kuanzia sasa ninaanza kuwapima kwa kusajili wananchi ambao hawapo kwenye mfumo rasmi wa ajira,ninataka vijana wengi wajiunge kwa wingi kwa kwa kujiunga kama kikundi na kujiunga na bima inayojulikana kama  ‘Kikoa” kwa kujiunga kikundi cha kuanzia watu kumi,wafikieni huko huko walipo
Kwa upande wa Mfuko wa Afya ya jamii(CHF) waziri huyo hivi sasa kuna CHF iliyoboreshwa hivyo kadi hiyo inatumika kwenye vituo vyote vya halmashauri  na si pale mwanachama alipokatia,”ni bora tuwachangishe elfu kumi kumi za watanzania ili tuweze kufikia usajili wananchi wengi na kupata huduma za afya bila vikwazo
Hata hivyo alishauri Manispaa hiyo kutengezea kadi ambayo itakua rafiki kwa mwanachama kuweza kuiweka kwenye waleti au mahali pengine ambayo itakua rahisi kwa kutunza na siyo kadi za hivi sasa ambayo ni mzigo kwa mwanachama kuibeba kwani kadi hiyo ni kubwa 
Aidha,alisema wizara yake inataka kuongeza gharama ya CHF iliyoboreshwa ya  shilingi elfu ishirini ambapo mwenye kadi hiyo ataenda kupata huduma hivyo hadi  hospitali ya mkoa,
“ tunazungumzia kila mtu apate huduma za tiba bila kikwazo,leo una hela,kesho huna na una umwa bora tunasema utoe elfu kumi na utibiwe ndani nya manispaa tena siyo peke yako bali na watu wako watano,alisema waziri ummy.
Hata hivyo alisema ni  marufuku  kwa mtu mwenye kadi ya CHF anapoenda kwenye vituo vya huduma ya afya kuambiwa akanunue kipimo au dawa bali wanatakiwa kupata vipimo vyote.

Comments