Featured Post

WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA NISHATI YA BIOGAS ILI KURAHISISHA MAISHA

Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas ,pamoja na wamiliki wa mitambo hiyo pamoja na mafundi Rowah Spear akiendelea kutoa elimu katika semina hiyo inayofanyika leo jiji hapa.
wakwanza kulia ni Mratibu wa Ubunifu  kutoka ECHO  Harold Msanya akiwa anafafanua jambo mbele ya wakufunzi hao
baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiendelea kufanya kazi ya majadiliano  katika makundi

Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas ndugu Rowah Spear akiwa anawaelekeza baadhi ya wadau waliouthuria semina jinsi biogas inaweza kufanya kazi
wadau wakiendelea kufatilia mada ilikuwa inaendelea



Mkurugenzi wa ECHO   Erwin Kinsey akiwa anaonyesha wakulima na wadau walioshiriki semina hiyo mmea aina ya gugukaroti ambalo ,alisema kuwa gugu ilo kwa asilimia 90% huku asilimia 10% ni gugu ambalo linaweza kutumika kutengeneza biogas(na woinde shizza,Arusha)
wadau wakiendelea na majadiliano katika makundi yao ikiwa ni sehemu ya kujifunza njia mbalimbali  na matumizi ya biogas
Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
Wananchi wametakiwa kutumia    Gesi Bayogesi  kwani  inapunguza gharama za watumiaji wa vyanzo vingine vya nishati  ,pia gesi hii inasaida kutunza mazingira .


Hayo yamebainishwa leo na Mratibu wa Ubunifu  kutoka ECHO  Harold Msanya wakati akitoa mada katika semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas , wamiliki wa mitambo hiyo pamoja na mafundi wanaofunga na kutengeneza mitambo hiyo .
 Alisema kuwa gharama za nishati ya umeme na gesi asilia ni ghali sana hasa kwa mtumiaji atakayedhamiria kutumia jiko la umeme au jiko la gesi lakini kwa gesi hii ya samadi mtumiaji  au mabaki ya nyasi aina mbalimbali zitamgharimu muda wake tu kujaza samadi na maji kila siku na atakuwa hana malipo ya pesa kila mwezi kama itakavyomlazimu kulipia umeme na gesi asilia kila mwezi, na hata kuni ambazo watumiaji wengine hununua

Alibainisha kuwa njia hii imeweza kuwasaidia na kuwapa faida baadhi ya wananchi ambao wameanza kutumia teknoligia hii na pia wengi wao wameshanufaika na huduma hii .
 Aidha Bayogesi ambayo aghalabu hutokana na kinyesi cha wanyama, masalia ya mimea na kinyesi cha binadamu inaweza kuzalishwa na kutumika kupikia na hata matumizi mengine kama vile kuendeshea mitambo mbalimbali.

“ Matumizi ya gesi hii kwa mtu ambaye ana mifugo kama vile nguruwe, ng’ombe yanaweza kusaidia kuondokana na gharama za kununua nishati ya kuni, mkaa, umeme na hata gesi asilia inayochimbwa ardhini.”alisema  Msanya
Kwa upande wake mkufunzi wa Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas ,pamoja na wamiliki wa mitambo hiyo pamoja na mafundi Rowah Spear alisemak uwa ni wajibu wa kila mtanzania kuwakikisha anakuwa na mtambo huo kwani mtambo huo unapunguza gharama   kubwa ambazo awali walikuwa wanatumia ,na pia pale mwananchi anapotumia mtambo huu anakuwa rafiki wa mazingira kwani kwanza kabisa akati miti ovyo na pili  yale majani ,vyakula ,na uchafu uchafu wa aina wowote anaweza kuukusanya na kuingiza katika mashina na ikamsaidia kupatikana kwa Biogas

Pia alisema kuwa mbali na kupata nishati yakupikia tu pia uchafu ambao unakuwa umetokana na mabaki haya unaweza kufanywa kama mbolea kwa mazao mbalimbali tunayoyalima hivyo ni vyema kila mwananchi kuhakikisha nyumbani kwake anamtambo huu

 

Comments