Featured Post

UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO WAWEKEWA MWONGOZO

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua  akizungumza na wajumbe wa Kikao cha Makatibu Wakuu cha Kupitia Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kilichofanyika tarehe 27 Julai, 2017 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo mjini Dodoma.

Baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha Makatibu Wakuu cha Kupitia Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani) alipokuwa akielezea lengo la Mwongozo huo Julai 27, 2017 Mjini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha Makatibu Wakuu cha Kupitia Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani) alipokuwa akielezea lengo la Mwongozo huo Julai 27, 2017 Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akionesha kitabu cha Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kwa wajumbe wa mkutano wa kupitia na kujadili mwongozo huo kilichofanyika Julai 27, 2017 katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw.Atupele Mwambene akiwasilisha Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwa wajumbe wa kikao cha kuujadili na kuupitisha mwongozo huo kilichofanyika tarehe 27 Julai, 2017 katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akipitia Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto wakati wa kikao cha kuujadili kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma Julai 27, 2017.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Obey Assery (wa kwanza kushoto) akifuatilia uwasilishwaji wa Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto wakati wa kikao cha kuupitia na kuujadili mwongozo huo kilichofanyika Julai 27, 2017 Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Zainabu Chaula akichangia hoja wakati wa kujadili Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika kikao cha Makatibu wakuu walipokutana kuujadili na kuupitisha mwongozo huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju akichangia hoja wakati wa kujadili Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto wakati wa kikao cha kuujadili mwongozo huo kilichjofanyika Julai 27, 2017 Dodoma.
Mkurugenzi wa Anuai za Jamii Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Anne Mazalla akiuliza swali kwa Mwenyekiti wa Kikao cha kujadili Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (hayupo pichani) Julai 27, 2017 katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Na Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua ameongoza kikao cha Makatibu Wakuu cha Kujadili na kuupitisha Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto nchini.

Kikao hicho kilichofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma Julai 27, 2017 ambapo kilihusisha Makatibu wakuu pamoja na wadau wa maendeleo kwa lengo la kujadili mwongozo huo ili kuhakikisha utekelezaji wake unaanza mapema iwezekanavyo.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Dkt. Mwinyimvua alieleza umuhimu wa mwongozo ikiwa ni nyenzo muhimu ya kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wanawake na watoto ambapo kabla ya kuandaliwa Mwongozo huo, Tanzania ilikuwa na mipango kazi minane (8) ya kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

“Lengo la Mwongozo huu ni kupunguza masuala ya ukatili kwa watoto na wanawake hivyo ni vyema ukajadiliwa na kuanza utekelezaji wake mapema ili kutatua changamoto za wanawake na watoto katika jamii.”Alisema Dkt.Mwinyimvua

Aidha mwongozo huo umeainisha mambo ya msingi yanayohusu masuala ya wanawake na watoto kwa kuangalia sheria mbalimbali zinazowalinda katika maisha yao ya kila siku ili kuwasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuzingatia haki na usawa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkingaamesema kuwa wanawake na watoto ndiyo wahanga wakubwa wa vitendo ya ukatili katika jamii hivyo Mwongozo huu ni nyenzo itakayoleta ufanisi katika kutatua vitendo vya ukatili dhidi yao na kuhakikisha haki na usawa vinakuwepo ndani ya jamii.

Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto nchini utaleta ufanisi na kusaidia masuala ya ukatili wa wanawake na watoto hapa nchini hivyo ni vyema kila mdau alione hili na kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na vita hii”.alisema Bi.Sihaba

Juhudi hizi zinafanyika ikiwa ni moja ya maadhimio ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, wakuu wa nchi wanachama ambapo kwa pamoja waliadhimia kutokomeza ukatili huo kupitia utekelezaji wa lengo Na. 5 na 6 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ifikapo 2030.

“Uwepo wa mwongozo huu utasaidia kupunguza athari za matokeo ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto angalau kwa asilimia 50 ili kundi hili liendelee kuchangia katika maendeleo ya nchi yetu”.Alisisitiza Bi.Sihaba

Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainabu Chaula alipongeza hatua zilizofikiwa na kuona kuwa ni mpango mzuri utakao fikia malengo yaliyokusudiwa ya kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini.

“Niipongeze Serikali kwa kuendelea na jitihada hizi ikiwemo kuwepo kwa mwongozo huu ambapo utatupa dira ya kuyafikia malengo yaliyokusudiwa juu mapambano ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto”.Alieleza Dkt. Zainabu.

AWALI:Mwongozo huo ulizinduliwa rasmi tarehe 13 Desemba, 2016 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto Ummy Mwalimu kwa niaba ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Jijini Dar es Salaam.

Comments