Featured Post

NMB YAZINDUWA SIKU YA WALIMU MKOANI DODOMA

Afisa Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (wa kwanza kulia) akifurahi pamoja na maofisa wa Benki ya NMB mara baada ya uzinduzi rasmi wa hafla ya siku ya walimu katika Mkoa wa Dodoma. Hafla ya uzinduzi wa siku ya Mwalimu ilifanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya hazini jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi wa NMB, Bw. Omari Mtiga (kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa siku ya Mwalimu katika mkoa wa Dodoma mwishoni mwa wiki.

Sehemu ya walimu waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa siku ya walimu mkoa wa Dodoma.

BENKI ya NMB imezindua rasmi siku ya walimu katika Mkoa wa Dodoma. Uzinduzi huo wa siku ya walimu Mkoa wa Dodoma ulizinduliwa rasmi na Afisa Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Jordan Rugimbana.
Hafla hii adhimu ilifanyika katika ukumbi wa Hazina na kuhudhuliwa na zaidi ya walimu 200 wa mkoa huo mwishoni mwa wiki. Uzinduzi wa hafla hii ni miongoni mwa mikakati ya NMB ya kuwafikia walimu nchini kote. Kusudi kubwa la hafla hiyo ya NMB na Walimu ni kuwaongezea uelewa walimu juu ya huduma za benki.
Hii ni kutokana na umuhimu wa kundi hili kubwa katika jamii inayotuzunguka. NMB wanaimani kwamba mwalimu akielimika jamii nzima itakua imepata elimu ya huduma za kifedha. Lakini pia kwa kuzingatia ukubwa wa kundi hili NMB imekua ikitumia fursa hii kupokea mrejesho ya jinsi huduma za kibenki zinavyopokelewa na wateja wake.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo mjini Dodoma, Meneja mwandamizi wa wateja binafsi wa NMB, Omari Mtiga alisema NMB inazo huduma mbalimbali ambazo kusudi lake kubwa ni kumsaidia mteja aweze kujikwamua kiuchumi. Aliongeza kuwa zipo huduma za mikopo ya aina mbalimbali ambapo walimu wanaweza kunufaika nayo.
Mikopo ambayo inatolewa na Benki ya NMB sio kwa ajili ya wafanyabiashara tu bali ni kwa ajili ya kila mtu mwenye vigezo vya kukopeshwa ambapo walimu ni miongoni mwa walengwa wa mikopo hii. Msichukue mkopo benki kama hamna mipango thabiti ya matumizi ya mkopo huo, Ni vyema kuchukua mkopo benki ukiwa na mipango endelevu," alisema Bw. Omari Mtiga.
"...Tukiwa kwenye mikakati ya serikali ya Viwanda ni vyema mkatumia vizuri maonyesho ya Nane nane yanayotarajiwa kuanza kutembelea mabanda ambayo mtajifunza namna ya uwekezaji kwenye sekta viwanda ili kujikwamua kiuchumi kwa kutumia uwepo wa benki ya NMB kwenye jamii yetu bila kuathiri mwenendo wa jaira zetu. Alisema kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge katika hafla hiyo.

Sehemu ya walimu waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa siku ya walimu mkoa wa Dodoma.
Picha za kumbukumbu na Sehemu ya walimu pamoja na Afisa Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge.

Comments