Featured Post

SBL YAZINDUA MRADI WA MAJI KWA WAKAZI WA CHANG'OMBE JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie (kulia), akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Chang'ombe B, Mgeni Hamisi Ramadhani wakati wa uzinduzi mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68  uliopo katika eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Miradi Endelevu wa SBL, Hawa Ladha. 


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie (kulia) na Diwani wa Kata ya Chang'ombe, Benjamini Ndalichako wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi huo.


Diwani wa Kata ya Chang'ombe, Benjamini Ndalichako , akisoma hutuba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo. Kulia ni Diwani wa Viti Maalumu, Mwanakombo Mwinyimvua na kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa katika eneo hilo.
Hii ni Crew nzima ya Kampuni ya Concept waratibu wa masuala yote ya mawasiliano ya SBL.
Mwonekano wa mradi huo.
Wananchi waliohudhuria hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, John Wanyanja akizungumza kwenye hafla hiyo kuhusu mradi huo.
Uzinduzi ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

 KAMPUNI ya Bia Serengeti leo imezindua  mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68  uliopo katika eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam  ikiwa ni jitihada za kuwaletea maji safi na salama wakazi wa eneo hilo.

Ukiwa na uwezo kwa  kuhudumia watu 4,000 mradi huo unajumuisha  kisima  pamoja na mifumo yake, pampu ya maji inayotumia nishati ya jua na tenki la maji  ambapo zinazalishwa lita 20,000 za maji kwa kila masaa ishirini na nne.

Akizungumza katika  hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Helene Weesie  alisema kuwa mradi huo ambao unajulikana, “Maji kwa Uhai” ni miongoni mwa  mikakati kama hiyo  ambayo kampuni ya bia  imeiendesha  katika mikoa ya  Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma ikiwa inawanufaisha  zaidi ya watu milioni moja kwa maji safi na salama.

 Weesie alisema kwamba mradi wa Chang’ombe  sio tu kwamba  utaboresha afya za wakazi wa eneo hilo bali pia  utaongeza tija kiuchumi, “hususani kwa watoto wa kike na wanawake  ambao  hawatahitaji kutumia saa nyingi  kutafuta maji safi sehemu nyingine. Hii inawapa fursa ya kuhudhuria shule wakiwa huru.”

 “SBL  ina sera iliyojikita katika ustawi wa jamii yetu na Maji kwa Uhai ikiwa ni mojawapo ya maeneo manne ya kipaumbele ambayo kampuni yetu imeyabainisha katika lengo lake  kuipatia jamii msaada katika jumuia inamohudumia”, alisema Weesie akielezea vipaumbele vingine hivyo kama: Kutoa Stadi za Maisha, Undelevu wa mazingira na Kuhamasisha Unywaji wa Kistaarabu.

Mkurugenzi huyo Mtedaji aliendelea kusema SBL ina programu ya kilimo  ambayo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita  imewasaidia wakulima zaidi ya 100 nchini kwa kuwapatia msaada wa kiufundi na kifedha iliyowasaaidia kuboresha maisha yao na maisha ya jumuia zao.

Weesie  alisema kutokana na juhudi hizo, “SBL imeweza kuibua tani za malighafi inazotumia kutoka wa wakulima wa hapa nchini kutoka 0 hadi tani 10,000 na hili limechangia  katika kukua kwa kampuni  na kukuza  kipato cha wakulima.”


Aliendelea kubainisha: “Licha ya kuchangia katika kukua kwa uchumi wa taifa  kupitia  malipo ya kodi ya mara kwa mara, SBL imetoa mchango muhimu katika maendeleo ya taifa hususani  katika kutoa  huduma  ya maji  safi na salama ndani ya nchi.”

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

Comments