Featured Post

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI NA KUZUIA MAKONTENA 20 YENYE MCHANGA WA MADINI ULIOKUWA USAFIRISHWE NJE YA NCHI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam kufatilia maagizo yake ya kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na wafanyabiashara wanaogiza na kusafirisha mizigo ndani na  nje ya nchi.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihesabu makontena 20 yenye mchanga wa madini ambapo ameamuru kontena hizo zisisafirishwe mahali popote.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa maagizo mbalimbali kuhusu makontena 20 (yanayoonekana nyuma)  yenye mchanga wa madiniuliokuwa usafirishwe kwenda  nje ya nchi ambapo ameagiza  Kontena hizo zisisafirishwe mahali popote.
Makontena 20 yenye mchanga wa madini yakiwa yamezuiwa kusafirishwa nje ya nchi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara alipofanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua nyaraka mbalimbali zenye maelezo kuhusu makontena ambayo husafirishwa nje ya nchi katika Bandari ya Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia baadhi ya magari yalivyoingizwa nchini na Wafanyabiashara wakubwa kwa njia isiyo halali ya kudai kuwa ni makontena ya mitumba wakati ndani yake wanaficha magari yakifahari wanayoyachanganya na bidhaa zilizochakaa.

Moja ya kontena likiwa lina gari ndani yake aina ya Range Rover ambapo muagizaji alidai kuwa anaagiza mitumba lakini kumbe ndani yake anakutwa ameficha magari ya kifahari.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na IGP Ernest Mangu mara baada ya kufanya ukaguzi Bandarini hapo. PICHA NA IKULU

Comments