Featured Post

MKWABI SUPERMARKET YATUMIA MILIONI 26 KUDHAMINI TANGA CITY MARATHON

Meneja Mkuu wa Mkwabi Group Of Campainers,Kawkab
Hussein akuzungumza na waandishi wa Habari leo kuhusu mashindano ya Riadha ya Tanga Marathon yatakayofanyika Aprili 15 mwaka huu ambayo yamefadhiliwa na Kampuni hiyo kwa kuwekeza kiasi cha sh.milioni 16 kushoto ni Mratibu wa Mashindano hayo Juma Mwajasho na Kulia ni Katibu wa Chama cha Riadhaa Mkoani Tanga(RT) Hassan Mwagomba

 Katibu wa Chama cha Riadhaa Mkoani Tanga(RT) Hassan Mwago mba akizungumza na waandishi wa habari leo kuishukuru kampuni ya Mkwambi Group of Campainers kufadhili mashindano ya Riadhaa Mkoani Tanga ya Tanga City  Marathon yatakayo fanyika April 15 mwaka huu katikati ni Mratibu wa Mashindano hayo Juma Mwajasho kulia ni Meneja Mkuu wa Mkwabi Group Of Campainers,Kawkab Hussein
Mratibu wa Mashindano hayo Juma Mwajasho akisistiza jambo kwenye mkutano na waandishi wa Habari Mkoanoi Tanga leo
 Sehemu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga wakiwa kwenye harakati za kuchukua matukio
 Sehemu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga wakiwa kwenye harakati za kuchukua matukio
Sehemu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga wakiwa kwenye harakati za kuchukua matukio
KAMPUNI ya Mkwabi Super Market imejitosa kudhamini Mashindano ya Tanga City Marathon kwa kuwekeza kiasi cha sh.milioni 16 ikiwa ni mkakati wa kurudisha hamasa na kuinua mchezo huo mkoani Tanga
Hatua ya Kampuni hiyo ambaye imekuwa mstari wa mbele kusaidia juhudi mbalimbali za michezo mkoani Tanga imelenga kurudisha hamasa na ushindani kwa washiriki.

Akizungumza na wandishi wa habari  leo Mratibu wa Mashi ndano hayo Juma Mwajasho alisema mbio hizo  zitaanza kutimua vumbi Aprili 15 mwaka huu katika Jiji la Tanga.

Mwajasho  alisema mashindano hayo yatasaidia kuongeza ari ya michezo na  kuamsha hamasa za wapenda riadha  katika mkoa wa Tanga na lengo ni kukuza michezo huo ambao utakuwa endelevu.

Alisema washiriki wa mashindano hayo kuanzia watoto wa miaka 12 kuendelea ambao  watakimbia mbio za kilometa tano,10,21, ambapo Mkwabi Super makert  .

Alisema mbio za kilometa tano fomu ya usajili itakuwa shilingi
1000,mbio za kilometa 10 sh 5,000 na mbio za kilometa 20 fomu itakuwa sh 8,000 ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha Tsh milion 10 na mshindi wa pili shilingi laki 700,000,mshindi wa tatu na wanne watapokea Tsh 500,000 na washindi wengine watapata kifuta jasho kila mmoja laki moja.

Katibu mkuu wa chama cha  riadha mkaoa wa Tanga Hassan Mwagomba alisema mashindano hayo kwao ni faraja  hivyo wameyapokea  kwa moyo nakwamba wataunga mkono juhudi hizo ili kuweza kufanikiwa mbio za Tanga City  marathoni mwaka huu wa 2017 .

Mwagomba alieza kuwa mashindano hayo ya mbio yataanzia  katika eneo la Mkwabi Super Makert  na kuzunguka  kwaminchi,kisha kuishia katika uwanja wa mkwakwani.

Alisema lengo kubwa la mashindano hayo ni kufufua riadha mkoani hapa ili kuweza kuleta mafanikio na yatashirikisha  wananchi wa mkoa mzima kwenye  halmashauri 11 na yatakuwa endelevu.

‘’Tunatarajia kupata wataalam  kutoka jijini Dar es salaam watakao wapima afya zao na usajili tayari umekwisha anza kwani zimebaki siku chache hivyo tuko kwenye hatua nzuri ya maandalizi’’alisema Mwagomba
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Comments