Featured Post

MKAZI WA KIJIJI CHA ISENGULE MKOANI KATAVI FATUMA ISSA (22) AJIFUNGUA WATOTO WANNE

Watoto wanne walizaliwa  na  mwanamke   aitwaye  Fatuma  Issa  22   Mkazi wa   Kijiji  cha  Isengule  Tarafa ya  Karema   mwambao  mwa  Ziwa   Tanganyika  Wilaya  ya  Tanganyika  Mkoa wa  Katavi wakiwa katika   chumba  maalumu  katika   Hospitali ya  Manispaa ya  Mpanda.

Huyu  ndiye  mwanamke   aitwaye   Fatuma  Issa  22  Mkazi wa  Kijiji  cha  Isengule   Tarafa ya  Karema   Wilaya  ya   Tanganyika    Mkoa wa  Katavi   akiwa   katika  chumba  maalumu  katika  Hospitali ya  Manispaa ya   Mpanda     baada ya kujifungua  watoto wanne kwa wakati mmoja  ambapo alijifungua  watoto hao  hapo machi 12  katika   Hospitali  hiyo  kati ya watoto hao mmoja ni wakike na watatu ni wakiume.

Mkuu  wa  Wilaya ya   Mpanda  Lilian  Matinga  akiwa  katika wodi ya  wazazi    katika   Hositali ya  Manispaa ya  Mpanda   aliwajulia  hali watoto wanne   mapacha  waliozaliwa hapo  Machi  12  mwaka huu kwa  wakati mmoja  na  mwanamke  aitwaye   Fatuma  issa  22   Mkazi wa  Kijiji  cha  Isengule  Tarafa ya  Karema  Wilaya ya  Tanganyika   Mkoa wa   Katavi
Picha  Na  Walter  Mguluchuma-Katavi yetu Blog


  Na  Walter  Mguluchuma .
    Katavi Yetu Blog
MKAZI wa kijiji cha Isengule , mwambao mwa Ziwa Tanganyika  katikawilaya ya Tanganyika  mkoani Katavi , Fatuma Issa (22) amejifungua watoto wanne katika Hospitali ya  Manispaa ya Mpanda mwishoni mwa wiki.

 
Muuguzi  Mkuu wa Hospitali hiyo , Alexanda Kasagula alisema mama huyo alijifungua watoto hao wanne mwishoni mwa wiki  kwa  njia ya kawaida ambapo mama na watoto wake hao  wote wakiwa na afya njema.

 
“Mtoto wa kwanza ambaye ni wa kike alizaliwa akiwa  na uzito wa kilo moja na gramu 800 ,mtoto wa  pili alizaliwa akiwa na uzito wa kilo moja na gramu 500 , watatu alizaliwa akiwa na uzito wa  kilo moja na gramu 800 huku wanne alizaliwa akiwa na kilo  moja na gramu 700.

 
Kati ya watoto hao watatu ni wakiume  hali ya mzazi na watoto wake wote  wanaendelea vizuri  bado wamelazwa  katika  wodi ya wazazi hospitalini hapa “ alieleza .

Kwa upande wake , Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Jafar Kitambwa alieeleza kuwa  mama huyo na watoto wake wataendelea  kuwa chini ya ungalizi hospitalini hapo  hadi hapo watakaporuhusiwa rasmi kwenda nyumbani

 
Mama huyo alieleza kuwa yeye na mume aitwae Agustino Andrew (25) kama wanando huo utakuwa uzao wao wa tatu ambapo wana idadi ya watoto watano .
 
“ Mie na mume wangu  sasa tuna idadi ya watoto  watano  uzazi wangu wa kwanza  nilizaa mtoto  mmoja ambaye yuko hai.Hii itakuwa mara yangu ya pili  kujifungua  watoto zaidi ya mmoja  katika uzao wangu wa pili   nilijifungua mapacha  lakini mmoja wao alikufa muda mfupi baada ya kuzaliwa na pacha mwenzake  alikufa  miezi mitatu  baada ya
kuzaliwa.

 
Nimejifungua watoto  wanne  lakini tangu nijifungue sijapata tatizo lolote la  kiafya  naendelea vizuri mie na watoto  wangu wote nawashukuru  wauguzi ambao wamenisaidia  hadi nimejiufungua salama bila ya matatizo yeyote yale “ alieleza
Alieleza kuwa  mama yake mzazi ndie anayemwangalia hospitalini hapo huku akimsadia kuwalea watoto hao .



Comments