KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) WILAYA YA MUFINDI JIMSON MHAGAMA AJITOSA UBUNGE WA AFRIKA MASHARIKI

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi, Jimson Mhagama, akiwa kwenye mmoja ya mikutano ya kampeni kumtafuta Diwani wa Kata ya Igombavanu wilayani Mufindi akikitumikia chama.

 Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi, Jimson Mhagama, akiwa kwenye mmoja ya mikutano ya kampeni akimwombea kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mwaka 2015 katika uwanjwa wa Wambi mjini Mafinga.
 Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi, Jimson Mhagama, akipeana mkono na Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne Mh. Mizengo Pinda kwenye moja ya majukumu ya kukitumikia chama.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi, Jimson Mhagama, akipeana mkono na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na kubadilishana maneno ya hapa na pale.

Na Fredy Mgunda, Mufindi
KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi, Jimson Mhagama, ametangaza nia ya kugombea nafsi ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwa kuiwakirisha Tanzania.
Akizungumza kwa njia ya simu Mhagama alisema kuwa atahakikisha lugha ya Kiswahili inatumika barani Afrika kama lugha mama kwa kuwa ndiyo lugha iliyosambaa zaidi barani humo.
“Nimetembelea nchi nyingi hapa Afrika nimekutana na watu wengi wanazungumza Kiswahili hivyo hoja yangu itakuwa kuhakikisha natimiza kitu alichotuachia hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,” alisema Mhagama.
Mhagama alisema kuwa atalazimika kuwatetea wakulima kwa kuwa asilimia kubwa ya Watanzania wengi ni wakulima na uchumi wao bado unategemea kilimo hivyo ni lazima kuwekeza nguvu kwenye kilimo chenye tija na kuinua mazao yanayozalishwa hapa nchi na kukuza uchumi.
“Tanzania tumebatika kuwa na ardhi nzuri na kubwa ambayo kwa asilimia kubwa bado haijatumika kwa mjibu wa wataalam wa kilimo hivyo ni lazima kutafuta njia mbadala ya kuwainua wakulima hawa ili kuviwezesha viwanda vyetu kupata malighafi nyingi na za kutosha ili kuinua kipato cha kila sekta hapa nchini,” alisema Mhagama.
Aidha, Mhagama amewataka Watanzania kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi anazozifanya kwa kutafuta njia bora ya kuinua uchumi wa wananchi wake kutoka hapa ulipo hadi kufikia uchumi wa viwanda kama sera yake alivyoielekeza kwenye Tanzania ya Viwanda.
“Angalia sasa tunapata wawekezaji wengi kwenye sekta ya viwanda, hii ni dalili nzuri ya kuukaribia uchumi wa viwanda, hivyo nikiwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki nitaendelea kuunga mkono juhudi za Rais kwa kutafuta njia za kuwainua wawekezaji wazawa ili waboreshe na kuanzisha viwanda vyao,” alisema Mhagama.
Mhagama aliwaomba Watanzania kwa ujumla kumuombea ashinde kiti hicho ili aweze kuiwakirisha vyema nchi kwa uadilifu uliotukuka.