HIVI NDIVYO ASKOFU GWAJIMA 'ALIVYOHUSIKA' KUISAMBARATISHA NDOA YA FLORA MBASHA. SOMA BARUA HII YA EMMANUEL MBASHA!
HII ni barua ya malalamiko aliyoiandika Emmanuel Mbasha, aliyekuwa mume wa mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora au ‘Madame Flora’, aliyoiandika mwaka 2014 na ikanaswa na vyombo vya habari na kusambaa kupitia mitandao ya kijamii kwenda kwa Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.

 Emmanuel Mbasha na mkewe Flora wakati wa mgogoro wa ndoa yao mwaka 2014. Huyu anaomba, huyu anatafakari!
Katika barua hiyo, ambayo MaendeleoVijijini inaichapa neno kwa neno, Mbasha alikuwa akilalamika Mchungaji (sasa Askofu???) Gwajima kuingilia na kuivuruga ndoa yake, ambayo kwa sasa imevunjika rasmi baada ya Flora kufungua madai ya talaka katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni na kushinda.
Mbasha, ambaye naye ni mwimbaji wa Injili, aliandika barua hiyo baada ya mgogoro kuendelea huku tuhuma nyingi zikielekezwa kwa Gwajima, kwamba ndiye aliyekuwa chanzo kutokana na kuwa na uhisiano wa kimapenzi na Flora licha ya kufahamu kwamba mwanamke huyo ni mke wa mtu.
Kumbe hata ile skendo ya Mbasha kubaka shemejiye ilikuwa ni ‘muvi’ iliyoandaliwa na Flora na Gwajima, kama hii ambayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alikuwa ameiandaa.
Na Mbasha anasema kwenye barua yake kwamba, kumbe waandishi watatu wa magazeti ya udaku walilipwa fedha ili kuhakikisha habari zinaandikwa katika ‘muvi’ hiyo na Mbasha anafungwa jela miaka 30 kwa ubakaji!
Hata suala la ‘sembe’ Mbasha amelidokeza kwenye barua yake, hivyo yawezekana tuhuma za sasa zilizozusha vita kati ya Gwajima na Makonda ni za muda mrefu na madai yamekuwa yakiendelea chini kwa chini.
Sitaki kukumalizia uhondo, barua hiyo inajieleza yenyewe hapa chini ingawa imehaririwa kwa makosa ya kisarufi tu:
"Mchungaji ... yapata kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya habari juu ya ‘utajiri' wa ghafla wa mke wangu mara baada ya mgogoro kutokea kati yangu na yeye, bila kupoteza muda mke wangu akanijibu kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa fedha kiasi cha milioni 9 na waumini kanisani kwako.

Mchungaji, naomba uelewe kuwa nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!! Kwanza ni kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mke wangu, lakini kiwango kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe rahisi kutimiza malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!!

Mnamo tarehe 3 mwezi Juni mwaka huu (2014), mlifungua akaunti mpya kwa jina la mke wangu katika benki ya CRDB Morogoro, na siku nne baadaye mke wangu aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18 kutoka akaunti ya MWANAMAPINDUZI FOUNDATION ambayo hiyo account ipo NMB Mwanza! Ambapo asasi hii inamilikiwa na mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu kutoka mikoa ya Kaskazini!

Nashukuru kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni kuwa kwanini kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie njia za siri ambazo si rahisi watu kujua kama mmempa fedha??

Pia napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi kuingizwa taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash zilitolewa na siku hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku ambao wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na aliyedeposit hizo fedha ni moja ya viongozi wako hapo kanisani!! Kuna nini hapo??

Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na mke wangu kwa muda mrefu sasa!

Binafsi nilianza kupata wasiwasi mwaka jana (2013) mwezi Desemba tulipoenda katika mkutano wako wa injili pale Morogoro! Mimi na mke wangu tulifikia hoteli ya Kingsway Msamvu na wewe ulifikia Nashera Hotel maeneo ya Forest Hill!!

Baada ya siku tatu za mahubiri mkutano wako ulipigwa marufuku na serikali kwa sababu ya maneno ya kichochezi uliyokuwa unahubiri, hivyo ikatulazimu waimbaji wote turejee Dar es Salaam!!

Lakini uliniomba mke wangu abaki na wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia watu maombi pale kanisani kwako Kihonda kwa muda wa siku nne!! Nilikubali na nikamuacha mke wangu nyumbani kwa dada yako pale Mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako alisafiri kwenda Mwanza na ikabidi mke wangu arudi hotelini Kingsway!!

Kwa taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale hotelini ni kuwa mke wangu hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa chumba kililipiwa kwa siku zote zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala wapi?? Je, unaweza kunieleza kwanini mke wangu alikuwa analetwa Nashera Hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi katika hili kwani hata namba ya dereva taxi ninayo!!

Yote haya nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea lakini nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa yangu isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala hamjishitukii sana sana mapenzi ndio yanazidi kuwa motomoto kati yenu!! Ulikuwa unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe mjinga kiasi gani? Nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa imefika point hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu Watanzania na dunia ikufahamu jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na unataka kuniziba mdomo kwa kunitishia jela miaka 30!!!

Wewe ni mpuuzi na shetani anaishi ndani yako... na nataka nikuahidi kitu kimoja kuwa NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako but at the end, I will be the last man standing!! Narudia tena, nitakushinda.!!

Bila kusahau naomba niongee na wewe pia mke wangu, hivi ni nini kilichokukuta ndani ya moyo wako How did we get here?? Je ni fedha zilizokufanya ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine?? Kama unanichukia mimi kiasi hiki je, uwahurumii hata watoto wetu?? Mbona tunawatengenezea mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama?? Hivi kisaikolojia hawa watoto watakuwaje? Si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na mikosi hii tunayowatengenezea? Kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa dhambi ambayo hawajaitenda?

Yes nafahamu nimekukosea mengi and am very sorry for that, lakini basi embu kumbuka mke wangu nimekuvumilia mambo mangapi mke wangu, kumbuka makosa mazito uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata ndugu yako ama ndugu yangu ili kulinda heshima yako!! Kumbuka jinsi tulivyopigana na changamoto mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja ya icons wa muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso, dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo hii tuko hapa!!!

Mke wangu, kwa miaka yote hii nimekubali nionekane Bushoke tu huku watu hawajui kuwa mimi ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi ndiye nimekuwa nafatilia na kufanikisha kila kitu chako from scratch!!!

Lakini nimekubali jamii inione Bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa na baadae!!! Nini kilichokubadilisha mke wangu? Fedha au huyo mchungaji mwanamazingaombwe?

Hivi kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili wanikandamize nionekane sifai katika jamii? Ni nini kilichokupata mke wangu??

Naomba uelewe kuwa binafsi siogopi kwenda jela kwa sababu ya hiyo muvi mliyonizushia, kwani ni bora nikakae jela kuliko kuishi huru huku mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu kama binadamu, lakini kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto wateseke kwa sababu ya tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana!

Najua kwa sasa inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na wewe kurudiana tena, lakini binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi kwani tumeharibu mno, lakini ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu upuuzi tunaoufanya sasa!!

Kumbuka hiki tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki wote wa Injili Tanzania, na tusipotubu tukajirudi Mungu atatuhukumu kwa dhambi hii!!

Kumbuka kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda katika hii vita, vyombo vya habari pekee ndivyo vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji wote tuta loose!!

Mwisho nimalizie na wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia kama kaka na kama mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye pembe saba, umeparaganyisha familia yangu, umeleta maumivu makali kwenye ukoo!!

Nakuonya tena kwa mara nyingine, muache mke wangu!! Huyo ni mke wangu, nilimtolea mahali mimi mwenyewe na wazazi wake waliniamini na kunikabidhi!!! Nasema niachie mke wangu!!

Wewe ni nyoka, imefika time Watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya kondoo!!!

Umedanganya watu vya kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa sababu ya kiburi cha pesa zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi cha kutosha imefika time tuwaeleze Watanzania ukweli na wakufahamu kuwa wewe ni nyoka!!

Sitakubali kuona ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na nitakushinda!!! Siogopi fedha zako wala connection ulizonazo, ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nimepiga magoti!

Nitapambana na wewe mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata wanangu wakiwa wakubwa wajue kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga magoti na kuelekeza shingo kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje familia yangu, bali licha ya umasikini wangu nilisimama kiume na kupigana kutetea familia yangu!!!

Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda.."
CHANZO: TAIFA KWANZA!