HATARI KWA WANAWAKE: JINSI JIKO UNALOPIKIA LINAVYOVURUGA HOMONI ZA KIKEFuatana nami Mkufunzi wako Amani Ezekiel - +255765366133

Wengi tunajua kwamba vyakula vingi vya viwandani vilivyowekwa kwenye makopo na makasha ya paketi si salama kwa 100%, na pia wengi hujua kwamba vinywaji laini na pombe sio salama kwa 100%, pia wengi tunajua sindano na vidonge vya uzazi wa mpango si salama kwa 100%. Pia vyakula vingi fresh vya kutoka nje ya nchi kama samaki, na nyama na cheese sio salama 100%.

Lakini wengi hatujui kama MAJIKO YETU si salama 100%. Mara nyingi huwa nasema ukiletewa chakula mezani, fikiria kidogo na jiulize swali hili ‘Je chakula nilacho kinaenda kuufanyaje mwili wangu”

ANGALIZO:
Wagonjwa wengi wa magonjwa sugu wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kwamba ametumia dawa flani ya kampuni flani akapata nafuu lakini hakuweza kupona kabisa. Akinamama kwa akinababa wengine pia walitumia mbinu mbalimbali za kupunguza uzito na kufanikiwa lakini baada ya muda uzito ulirudi tena mara mbili zaidi.
Swali ni kwamba nini shida. Jibu ni rahisi sana Ukishatibiwa malaria unatakiwa ulale kwenye net sio ulale bila net, ukilala nje ya net utapata malaria tena. Ndio hata magonjwa sugu ukishatibika/kupata nafuu basi unatakiwa uache baadhi ya vitu vilivyopelekea wewe kupata magonjwa hayo.

DALILI KWAMBA HOMONI ZA MWANAMKE ZIMEVURUGIKA

1. Kuwa na hedhi ya muda mrefu zaidi ya siku 7
2. Kuwa na hedhi yenye kuambatana na maumivu Makali sana
3. Kuwa na hedhi yenye kuambatana na kichefu chefu na kuharisha
4. Kuwa na hedhi iliyojaa woga mkubwa sana
5. Kuwa na hedhi ambayo haina mpangilio, Unaweza kuingia mara tatu kwa mwezi mmoja, mara mbili au unaweza usipate kabisa hata miezi 6 hadi mwaka.
6. Kuwa na ndevu sehemu za usoni na kifuani nyingi kupita kiasi
7. Kuwa na kitambi cha tumbo la chini (Abdominal obesity)
8. Kukosa mtoto kwa muda mrefu
9. Kukosa hamu ya tendo la ndoa na kuwa na tendo la ndoa lenye kuambatana na maumivu makali
10. Mwili kuwa unauma sana hasa misuli bila sababu ya msingi, kuumwa sana na kichwa bila sababu ya msingi.

HOMONI NI VITU GANI


Homoni ni kemikali zinazotolewa na tezi za mwili na kusafiri mwilini kupitia mfumo wa mzunguko wa damu hadi ogani za mwili. Homoni ndio zinasababisha mabadiliko katika ogani mbalimbali za mwili. Kwa lugha nyingine zinapeleka ujumbe kwa ogani mbalimbali za mwili ili ziweze kufanya kazi kulingana na mahitaji ya mwili.
Homoni ndio kemikali kuu zinazotumika kusafirisha taarifa kwenye viungo mbalimbali vya mwili hivyo mabadiliko madogo ya homoni husababisha mabadiliko makubwa kwenye mwili.
Mfumo wa utengenezaji wa homoni unalingana kwa kiasi kikubwa kwa wanaume na wanawake isipokuwa homoni zinazotengenezwa kwenye tezi zilizopo kwenye mfumo wa uzazi.

Baadhi ya Homoni na Kazi zake
1. Homoni ya KiumeTestosteroni, homoni hii huhusika na uumbaji wa via vya uzazi tangu mtoto akiwa tumboni, inabalehesha na pia kumpa mwanaume nguvu na hamu za tendo la ndoa.Katika mwili wa mwanamke homoni hii ipo kidogo sana.
2. Homoni ya KikeOestrogen, homoni hii huhusika na uumbaji wa via vya uzazi vya mwanamke tangu akiwa tumboni, inabalehesha na pia inahusika na mzunguko wa hedhi na kumpa mwanamke hamu ya tendo la ndoa.
3. Homoni ya Insulini – homoni hii ipo kwa wanaume na wanawake inahusika na kupunguza kiasi cha wanga na sukari (glucose) katika mfumo wa damu.

NAMNA HOMONI ZINAVYOVURUGWA
 
Miili yetu ikiwa katika hali ya kawaida hutengeneza homoni kwa uwiano stahiki na kufanya ogani na tishu za mwili kufanya kazi vizuri.
Pale homoni moja au zaidi inapoongezeka au kupungua kiwango cha kawaida kinachohitajika na ogani/tishu ili kuweza kufanya kazi basi na homoni zingine huongeza au kupunguza uzalishaji wake.
Baadhi ya sababu zinazopelekea kuvurugika kwa hormone mwilini.
- mifumo ya uzazi wa mpango wa kisasa (vidonge na vijiti)
- msongo wa mawazo
- matumizi makubwa yaliyopitiliza ya vipodozi.
- ujauzito, kukoma kwa hedhi kwa wanawake kutokana na umri
- kubale/kuvunja ungo
- kutokufanya mazoezi
- mfumo wa maisha, unene, na mfumo wa ulaji (kula wanga na sukari ile hali wanga huo hauendi kutumika)

MWANAMKE: MAHUSIANO YA CHAKULA UNACHOKULA NA UZAZI

MATOKEO YA UPIKAJI WA WANGA NA UTUMIAJI WA SUKARI NYINGI JIKONI
1. KUONGEZEKA KIASI CHA HOMONI YA KIUME KWA MWANAMKE:
Ulaji wa wanga na sukari nyingi ile hali mwanamke hauko na kazi nyingi za kufanya, yaani wewe unakuwa umekaa tuu tangu asubuhi husafishi nyumba, wala, nguo, wala vyombo, kazini kwenyewe wewe ni bosi, hufanyi mazoezi wala kazi ngumu za mikono, hii inapelekea mwanamke kuwa mnene na mzito hivyo kuwa na kiasi kikubwa cha homoni ya insulin mwilini.
Homoni hii ya insulin ikishakuwa nyingi mwilini kwa mwanamke inasababisha kuongezeka uzalishaji wa homoni ya kiume (Kwa kawaida homoni hii ipo kiasi kidogo ndani ya mwili wa mwanamke). Matokeo yake angalia kipengere (a) na (b) hapa chini:
(a) Ikiwa homoni ya kiume itakuwa nyingi ndani ya mwili wa mwanamke matokeo yake ni mwili wa mwanamke kugeuka na kuwa na tabia za kidumedume (Kuota ndevu, kuwa na sauti neno, kuota chunusu sugu, kunenepa sana na kuwa na kitambi katika tumbo la chini). Kuna hatari pia ya kupata kisukari aina ya II. Pia unakuta mwanamke ana uso wenye mafuta mengi sana kupita kiasi, shingo kuwa nyeusi sana na sehemu zingine kama kwapa na kwenye mikunjo sehemu za siri, kupata viotea shingoni yaani “Skin Tags”.

MUHIMU TAMBUA YA KWAMBA – Ulaji wa Wanga na Sukari uliopitiliza ile hali huna kazi za nguvu inapelekea mwanamke kushindwa kukomaza mayai yake, hii ni kutokana na kuongezeke kwa kiwango cha insulin mwilini ambayo inaenda kuamsha uzalishaji homoni ya kiume inayomfanya mwanamke awe na mwili wa kidumedume.
TAKE NOTE: Si wanawake wote watapatwa na matatizo haya hata kama wanakula wanga na sukari kwa wingi na hawana kazi za nguvu, hii ni kwa sababu kila mwanamke ana mwili wake tofauti na mwingine (kila machine ina ufunguo wake)
(b) KUSHINDWA KUPEVUSHA MAYAI Mwanamke huwa ana viwanda viwili vya kuzalisha mayai kila mwezi yaani kwa lugha nyingine ni “Ovari ya kushoto” na “Ovari ya kulia”.
Ndani ya ovari ya mwanamke kuna mayai ambayo hayajakoma. Haya mayai hukomazwa kila mwezi na kutupatia yai ambalo linatakiwa lipatiwe urutibishaji endapo itakutana na mbegu ya kiume.
Sasa inapotokea hizo mifuko ya mayai zimekomaa vizuri kwenye ovary na zinatakiwa zipasuke zitoe mayai NA KWA BAHATI MBAYA kabisa “Kitendo hicho kinashindikana” hivyo hizo mifuko ambazo zimeshindwa kupasuka na kutoa yai zinabaki na umbo kama “Zabibu zilizo kwenye kikonyo chake”.
Kwa hiyo katika mji wa uzazi kuna kuwa na alama nyingi kama za zabibu hivi zimejaa.
2. KUONGEZEKA KWA KIASI KIKUBWA CHA HOMONI YA KIKE KWENYE MWILI WA MWANAMKE
Kiwango cha Estrogen (homoni ya kike) huongezeka kupita kiasi
Hii inasababishwa na insulin kuisisimua ovary kufanya kazi kwa kiwango kikubwa na hii inapelekea kiwango cha homoni hii kuwa juu kwenye damu.
Madhara ya homoni hii kuwa katika kiwango kikubwa katika mwili inaweza kukupelekea ukuta wa kizazi kujengeka na kuwa mnene kupita kiasi na hatimaye unaweza kuwa hatarini kupata kansa ya kizazi.
Na hii ndio sababu kubwa ya kupata hedhi nzito kupita kiasi yenye mabonge ya damu sana, kwa sababu kazi kubwa ya homoni ya kike ni kukufanya wewe uonekane “mwanamke” na ndio homoni ambayo inajenga ukuta wa kizazi kila mwezi ili kama mimba ikitungwa mtoto aje ajishikize kwenye ukuta imara.
Lakini inapotokea kiwango chake ni kukubwa ukuta mnene utajengwa kila mwezi na inapokuwa mimba haijatungwa ukuta utabomolewa na kama ukuta huu ni mnene wakati wa hedhi ya kawaida damu nyingi sana itatoka. Ukiona dalili hizo fika hospitali maana kuna hatari kubwa ya kuishiwa damu.

USHAURI
KAMA UNA DALILI HIZO HAPO JUU NA KISHA ULIPATA DAWA HOSPITALINI NA HUJAPONA, mchawi wako anaweza kuwa jiko lako. Watu wengi wanene walikokuwa katika program yetu ya kupunguza unene na vitambi wametoa shuhuda nyingi sana za kuwa wepesi wa mwili, kupata hedhi kawaida na pia kuwa wachangamfu wakati wa tendo la ndoa.
UNAWEZA PATA BIDHAA NA HUDUMA ZIFUATAZO TOKA TREVO
1. Program ya kupunguza unene, uzito na kiriba Tumbo pamoja na kurudisha hedhi iliyovurugika (kwa muda wa miezi mitatu. Trevo, itakufikia popote ulipo ili mradi una WhatsApp utapata program.
2. Program ya kukontrol kisukari bila kutumia insulin injection, hii ni ndani ya siku 90 utakuwa upo vizuri na baada ya hapo utajifunza namna ya kuishi bila kutegemea sindano. (inawahusu wanaume na wanawake), pia utaipata popote ulipo duniani.
3. Waliokosa watoto muda mrefu nenda kapime hospitalini ijulikane shida ni nini, je ni uvimbe, mayai machanga, mbegu hazina nguvu, ukuta wa mimba mbovu? Suluhisho lipo.

Whatsapp +255765366133 na Massage za kawaida
 Simu tu      +255 716128536

MAJI NA MAZOEZI NI MUHIMU SANA, mana wengine katika program yetu ya kula huacha kufanya mazoezi, fanya mazoezi mepesi ya kutembea, kukimbia taratibu (jogging), kuendesha baiskeli, sitt ups na mazoezi ya kazi ndogondogo za mikono. Ni LAZIMA kwa mwanadamu uliye hai ili uongeze uwezo wa mwili wako kuchakata chakula na kuchukua vitaminis, madini na nguvu pamoja na nishati mbalimbali kwa ajii ya ujenzi wa mwili wako.

UKIKAA IDLE VITU VINGI MWILINI MWAKO VINAKUWA IDDLE.

Credit: Mitandao ya Kijamii