Featured Post

TIGO YAZINDUA KIFURUSHI KISICHO ISHA MUDA CHA 'HALICHACHI'


 Meneja Chapa wa Tigo,  William Mpinga (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa kifurishi kisicho isha muda cha halichachi. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael.


 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.


 Mkutano ukiendelea.


Wapiga picha wakichukua taarifa hiyo.



KAMPUNI ya Tigo Tanzania leo imetangaza  kuanzishwa kwa  ubunifu mwingine wa kifurushi cha data na sauti  ili kukabiliana na hitaji la wateja. Kifurushi kipya kinajulikana kama ‘Halichachi’ (Muda wake hauishi) na ni mwendelezo  wa kujikita kwa Tigo  katika kuwapatia wateja wake  uhuru wa mawasiliano.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari leo wakati akitangaza kampeni hiyo mpya   Meneja Chapa wa Tigo William Mpinga alisema, “Tuna furaha  kubwa wakati kampuni inazindua  kifurushi kipya  ambacho kitawahakikishia wateja wake kwamba wanakuwa na mamlaka ya kumiliki vifurushi vyao   wakati muda wa kumalizika kwa kifurushi haitakuwa  ni changamoto tena.”
  
“Ni dhahiri kuwa soko la mawasiliano ya simu  linakua  ambapo  huduma za mawasiliano ya simu za mkononi  zinaongezeka kwa mrengo wa  kununua vifurushi,” alisema Mpinga na kuongeza, “Tunazindua kifurushi cha kipekee  tukiwa tunajiamini kwamba  kitakuwa ni  suluhisho sahihi kwa wateja wetu.

“Kifurushi hiki kinaingia katika soko ikiwa ni  sehemu ya mtiririko wa ubunifu uliowekwa ili kuhakikisha kwamba tunasimamia mtazamo wetu  katika kutoa huduma nzuri kwa wateja wetu. 

Tunaamini kwamba  kifurushi hiki ni kiashiria kilicho wazi kwamba tunaongoza katika kutoa masuluhisho ya mawasiliano ya simu  yaliyo na ufanisi nchini Tanzania.”

Kifurushi hiki kipya  ni sehemu ya mkakati wa Tigo wa kutoa huduma ndani ya safari yake ya ubunifu na miongoni mwake  ikiwa ni kuanzishwa kwa  huduma ya bure ya WhatsApp, Facebook ya Kiswahili  na YouTube  ambayo kampuni ilizindua mwaka 2016.

Comments