Featured Post

TAKWIMU ZINAZOONESHA HALI YA UZAZI SALAMA NCHINI TANZANIA





 Karibia wanawake 67,000 walitibiwa katika vituo vya afya kwa ajili ya matatizo yanayotokana na utoaji mimba usio salama kwa mwaka 2013 nchini Tanzania. Hata hivyo, karibu wanawake wengine 100,000 ambao walipata matatizo yaliyohitaji tiba katika kituo cha afya hawakupata matibabu waliyohitaji. (Chanzo: guttmacher.org)







Inakadiriwa kuwa, mimba 405,000 zilitolewa ndani ya mwaka 2013 nchini Tanzania. Idadi hii ni kiwango cha utoaji wa mimba 36 kwa kila wanawake 1,000 wenye umri kati ya miaka 15-49 na uwiano wa utoaji mimba 21 kwa kila watoto 100 wanaozaliwa wakiwa hai.

•Nchini Tanzania, viwango vya utoaji mimba hutofautiana sana kwa ukanda, kutoka 11 kwa wanawake 1,000 kwa Zanzibar hadi 47 kwa Nyanda za Juu Kusini na 51 kwa Kanda ya Ziwa. Ukanda wa Ziwa na Nyanda za Juu Kusini huwa na viwango vya juu vya matibabu kwa matatizo yatokanayo na utoaji mimba pia.

 •Mwaka 2013, katika nchi nzima, 15% ya mimba zilitolewa, 52% katika uzazi uliokusudiwa, 18% katika uzazi usiokusudiwa na 15% katika mimba zilizoharibika. Mgawanyo huu hutofautiana kwa maeneo kwa mfano, uwiano wa mimba zilizotolewa ni kati ya 6% kwa Zanzibar hadi 18% kwa Nyanda za Juu Kusini.
(Chanzo: guttmacher.org)



 Kupunguza utoaji mimba usio salama na vifo vya wajawazito na majeraha yanayohusishwa na utoaji mimba, utahitaji kupanua upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango ili kuzuia mimba zisizotarajiwa, na kupanua upatikanaji wa huduma za baada ya kuharibika kwa mimba.

 Vituo vya afya katika ngazi zote lazima viwe na dawa muhimu za kutosha, vifaa vya kutolea huduma za msingi za baada ya kuharibika kwa mimba, na watoa huduma wa kawaida wanapaswa wapewe mafunzo ya kutoa huduma hizo.

Utata kuhusu sheria ya utoaji mimba ya Tanzania unatakiwa ufafanuliwe ili kusaidia kuunga mkono taratibu salama na kisheria zitumike kikamilifu, na kuhakikisha kuwa wanawake hawana sababu ya kuamua kutumia njia zisizo salama kutoa mimba zao. 
(Chanzo: guttmacher.org)

Comments