Featured Post

WANAUME KENYA KUNYIMWA TENDO LA NDOA NA WAKE ZAO KAMA HAWATAJIANDIKISHA KWAJILI YA KUPIGA KURA




Mbunge mmoja ametoa wito kwa wanawake waliopo katika maeneo yenye wafuasi wengi wa upinzani nchini Kenya kutofanya mapenzi na waume zao ambao hawajajisajili kama wapiga kura.

Kwa mujibu wa gazeti la The Standard nchini humo, mwakilishi wa wanawake mjini Mombasa Mishi Mboko amewataka wanawake nchini humo kuwanyima wanaume zao haki zao za kindoa ili kuwashinikiza waende kujisajili kama wapiga kura ili kujiandaa kwa uchaguzi wa mkuu ujo unaofanyika tarehe 8 mwezi Agosti.
Akiongea katika uwanja wa maonyesho ya kilimo katika eneo la Mkomani Bi Mboko alisema kuwa ngono ni kifaa kizuri kinachoweza kuwashinikiza wanaume kukimbilia kujisajili katika shughuli hiyo ilionza siku ya Jumatatu.
Kulingana na gazeti hilo hata hivyo, mumewe Mboko hatonyimwa haki hiyo ya ndoa kwa kuwa tayari amejisajili kama mpiga kura.
“Wanawake huu ndio mpango munaofaa kuutumia.Ni mpango muziri sana.Wanyimeni haki yao ya kufanya mapenzi hadi pale watakapowaonyesha cheti cha kupiga kura”, alisema.
Mboko aliongezea kwamba imefikia wakati ambapo wanawake wanafaa kutumia ngono kuwalazimisha waume zao kuchukulia shughuli ya usajili wa wapiga kura na umuhimu mkubwa.
Source: BBC

Comments