VIDEO - WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUUNDA VIKUNDI WAWEZE KUJIUNGA NA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF) ILI KURAHISISHA UPATIKANAJI WA MATIBABU

Wajasiriamali toka vikundi mbalimbali mkoani Ruvuma wamehamasishwa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili kurahisisha matibabu wawapo katika shughuli zao za kawaida, Wajasiriamali watakaojiunga na mfuko huo na kuwa wanachama watalipia shilingi 76,800 kwa mwaka ili kupata matibabu kupitia mfuko huo.