Featured Post

TANZANIA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KUHARAKISHA MAENDELEO YA NCHI



Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto), akiwa katika mazungumzo na mgeni wake ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, walipokutana Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (katikati) pamoja na maafisa waandamizi wa Wizara hiyo wakiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, (kulia) akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo kati yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dares salaam ambapo IMF imeipongeza Tanzania kwa kusimamia vizuri ukuaji wake wa uchumi.

Ujumbe wa Tanzania na Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF wakiwa katika mazungumzo Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam, ambapo Shirika hilo limeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania ili kufikia maendeleo inayoyatarajia kwa manufaa ya Taifa na wananchi wake kiuchumi na kijamii.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani), Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dares salaam ambapo IMF imeipongeza Tanzania kwa kusimamia kikamilifu ukuaji wake wa uchumi.

Mkurugenzi wa Idara ya Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ollal, akisisitiza jambo wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, walipokutana Makao Makuu ya Wizara hiyo, Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akizungumza jambo na mgeni wake ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, (hayupo pichani), Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akizungumza jambo na mgeni wake ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, (hayupo pichani), Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto), akiagana na mgeni wake ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam, ambapo IMF, imesifu jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano, katika kusimamia na kukuza uchumi wa Taifa.

Benny Mwaipaja
WFM-Dar es salaam

SERIKALI imesema kuwa inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi wa nchi na kuahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano na sekta hiyo ili kuharakisha maendeleo ya wananchi kupitia sekta ya viwanda na biashara.

Hayo yamesema na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa uchumi wa nchi unategemea sana sekta binafsi yenye nguvu na yenye utulivu ambayo itachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi kwa njia ya uwekezaji na ulipaji kodi.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, amesema kuwa Shirika lake limeridhika na kiwango kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa Tanzania miongoni mwa nchi za Afrika na kwamba wanatarajia kuona uchumi huo ukiendelea kukua zaidi kwa ushirikiano na sekta binafsi.

Ametaja sifa za ukuaji huo kuwa ni pamoja na kuimarishwa kwa ukusanyaji wa kodi, udhibiti wa mfumuko wa bei na thamani ya shilingi, uwajibikaji na pamambano dhidi ya rushwa, ufisadi, na utekelezaji mzuri wa  Bajeti ya serikali.

Hivi karibuni Bodi ya Wakurugenzi ya IMF ilitoa taarifa yake ya mapitio ya mwenendo wa uchumi wa Tanzania na kueleza kuridhika kwake na uimara wa uchumi huo baada ya kutoyumba katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 na kueleza kuwa utaendelea kukua kwa wastani wa asilimia 7 kama ilivyopangwa.

Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani ni chombo cha kimataifa kinachosaidia ukuaji wa uchumi wa nchi wanachama wake kwa kuweka mikakati na kuzikopesha fedha kwaajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ya kiuchmi na kijamii ikiwemo, elimu, afya, miundombinu, nishati na miradi mingine kadha wa kadha.

Mwisho






Comments