Featured Post

NAIBU WAZIRI MASAUNI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI JIJINI MBEYA

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na maafisa wa Jeshi la Polisi alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kubaini mafanikio na changamoto za jeshi hilo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisikiliza maelezo juu ya gari lililokamatwa likisafirisha wahamiaji haramu   kutoka kwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benjamini Kaizaga(aliyenyoosha mkono).Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benjamini Kaizaga, juu ya gari  lililokamatwa likisafirisha madawa ya kulevya.Wengine mstari wa mbele  ni   Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula(wapili kulia)  na  Naibu Kamishna wa Uhamiaji,Asumsio Achachaa .Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia), akifurahia jambo wakati alipotembelea makazi ya mbwa wanaotumika na Jeshi la Polisi katika masuala ya ulinzi na usalama.Baada ya Naibu Waziri ni Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya,Emmanuel Lukula. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipanda mti katika makazi ya mbwa wanaotumika katika masuala ya ulinzi na usalama na Jeshi la Polisi.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


Comments