Featured Post

MAKAMU WA RAIS APOKEA TAARIFA YA TATHMINI YA UJENZI WA BOMBA JIPYA LA MAFUTA SAFI LA TAZAMA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasikiliza Mawaziri wa Nishati kutoka Tanzania na Zambia wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya tathmini ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta safi kutoka Tanzania mpaka Zambia, Mawaziri hao ni Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Mhe.Profesa  Sospeter Muhongo (kulia) na Waziri wa Nishati wa Zambia Bw. David Mabumba (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Mhe.Profesa  Sospeter Muhongo (kulia) na Waziri wa Nishati wa Zambia Bw. David Mabumba (kushoto) mara baada ya kumaliza mkutano wa kumpa taarifa Makamu wa Rais ya tathmini ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta safi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Nishati wa Zambia Bw. David Mabumba (kushoto) mara baada ya kupokea taarifa  ya tathmini ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta safi litakalotoka Dar es Salaam, Tanzania mpaka Ndola, Zambia, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Tanzania na Zambia ambao ulifanya ziara ya kukagua pampu na bomba la mafuta la TAZAMA kutoka Ndola, Zambia mpaka Dar es Salaam Tanzania wakiongozwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Nishati wa Zambia Bw. David Mabumba ambapo walifanya tathmini ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta safi litakalotoka Dar es Salaam, Tanzania mpaka Ndola, Zambia.

Comments