Featured Post

DK. KIGWANGALLA ATOA SIKU 7 KWA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA KUMALIZA CHANGAMOTO ZINAZOIKUMBA HOSPITALI YA RUFAA YA KITETE



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa siku siku 7  kwa Katibu Mkuu kumaliza changamoto zinazoikumba hospitali ya Rufaa ya Kitete iliyopo mkoani Tabora.
Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo alipofanya  ziara ya kushtukiza  katika hospitali ya Rufaa ya Kitete Mkoani Tabora na kukagua miradi ya  chumba cha upasuaji  pamoja na Chuo cha AMOS kilichopo mkoani humo.

“Chumba hiki cha upasuaji na  Chuo vimekamilika mpaka thamani za ndani tangu miaka miwili iliyopita Sababu ni kwamba Serikali yetu haikutoa counter-part funding huku Benki ya Maendeleo ya Afrika  ikiwa imetimiza ahadi yake kwa asilimia mia moja”alisema Dkt. Kigwangalla. 
Hata hivyo Dkt. Kigwangalla amesema kuwa amefurahishwa kutekelezwa kwa baadhi ya maagizo aliyoyatoa  kama vile  kuondoa msongamano wa wagonjwa kwenye wodi za wanawake wajawazito na watoto.
Kwa mujibu wa Dkt. Kigwangalla amesema kuwa uongozi wa Hospitali hiyo umefanikiwa  kuboresha huduma ya upatikanaji wa dawa zote muhimu na huduma kwa wateja ikiwemo  lugha nzuri kutoka kwa wahudumu imeboreshwa..
Aidha Dkt. Kigwangalla amesema anashukuru uongozi wa Hospitali hiyo kwa kufanya ukarabati mkubwa wa majengo ya wodi za wagonjwa na sasa hakuna tena msongamano na huduma zinatoka kwa wakati sahihi.

Comments