Featured Post

BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUKUZA UCHUMI

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa Pili kutoka kulia) akisisitiza jambo wakati wa alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia ukanda wa Afrika Bw. Makhtar Diop, makao makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar salaam.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop, (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Wizara na Taasisi zake baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati yake na mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Makao Makuu ya Wizara hiyo, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiagana na Mgeni wake, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop, mara baada ya kumalizika kwamazungumzo kati yao, ambapo Benki hiyo imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuipatia Mikopo yenye mashari Nafuu kwaajili ya miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop, akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), walipokutana kwaajili ya mazungumzo Makao makuu ya Wizara hiyo, Jijini Dar es salaam. Wanao shuhudia ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anaye hudumia nchi za Tanzania, Malawi, Burundi, Bella Bird na Msaidizi wa Waziri wa Fedha na Mipango, Bw. Edwin Makamba (aliyesimama)
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (Kushoto) akizungumza na mgeni wake, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia kanda yas Afrika, Bw, Makhtar Diop, (wa kwanza kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anaye hudumia nchi za Tanzania, Malawi, Burundi, Bella Bird, na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James.
Ujumbe wa Tanzania na Benki ya Dunia, ukiwa katika kikao kilichojadili masuala mbalimbali yanayogusa Serikali na Benki hiyo, wakiongozwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop, pamoja na Mwenyeji wake,  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango,Jijini Dar es salaam,
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (Wa Pili kulia), akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop, Makao makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Watendaji wakuu wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wakiwa katika Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop ( hawapo Pichani), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
(Picha na Kitengo cha cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

NA BEN MWAIPAJA -WFM
DAR ES SALAAM, 25 JAN 2017    
BENKI ya Dunia imekubali kuikopesha Tanzania fedha kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo mkopo wa Dola Milioni 350 kwa ajili ya Mradi wa Upanuzi wa Bandari ya Dar es salam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dokta Philip Mpango, amewaambia waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika kwa Mazungumzo kati yake na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anaye shughulikia Kanda ya Afrika, Mhe. Makhtar Diop, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa kukamilika kwa upanuzi wa Babdari hiyo kutasaidia kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa na Bandari hiyo hatua itakayo chochea ukuaji wa  uchumi wa nchi.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Mhe. Makhtar Diop, amesema kuwa Benki yake imefurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano katika kukuza uchumi na kwamba Benki hiyo itaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha kuwa malengo yaliyokusudiwa yana fikiwa kwa haraka
Ameishauri Serikali kuongeza ushirikiano kati yake na Sekta Binafsi katika kuchochea  biashara na uwekezaji pamoja na kutupia jicho sekta ya kilimo kwa kuboresha uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo pamoja na kuongeza thamani ya mazao hayo ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kuondokana na umasikini na kuchochea uwekezaji katika sekta hiyo

Comments