Featured Post

NDOA YA UPEPO YAFUNGWA TENA JIJINI MBEYA

Bwanaharusi Ndugu Samwel Makalobo akivishwa pete ya ndoa na Mke wake Given Mgaya katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Isanga jijini Mbeya .Picha na Keneth Ngelesi .

 JamiiMojaBlog,Mbeya
HATIMAYE lile tukio lililovuta hisia za watu wengi la bibi harusi, Given Mgaya, kukimbiwa kanisani na mchumba wake siku ya harusi, limepatiwa jibu baada ya bwana harusi , Samwel Mwakalobo, kujirudi na kuamua kutimiza ahadi yake ya kufunga ndoa.
Ndoa hiyo imefungwa leo  majira ya saa tisa Desemba 23  katika Kanisa la (K.K.K.T) Usharika wa Isanga na kufungishwa na Mchungaji, Mathias Andangile Mwakijungu, huku tukio hilo likishuhudiwa na idadi kubwa ya waumini na wananchi wa kawaida waliojitokeza kanisani hapo.
 Kabla ya  maharusi hao kula kiapo cha ndoa,Mchungaji Mwaijungu alitumia zaidi ya saa moja kutoa nasaha kwa maharusi kutokana na tukio lilotokea awali Disemba 16 mwaka huu baada ya Bwana harusi kuingia mitini bila kutoa sababu zozote.

Bwanaharusi akisaini hati ya Ndoa mbele ya mchungaji wa kanisa hilo Ndugu Mathias Mwaijungu mara baada ya ndoa hiyo kufungwa rasmi Desemba 23  mwaka huu.

Bibi harusi akisaini hati ya Ndoa mbele ya mchungaji wa kanisa hilo Ndugu Mathias Mwaijungu mara baada ya ndoa hiyo kufungwa rasmi Desemba 23  mwaka huu.

Mbali na kutoa nasaha kwa maharusi,pia Mchungaji Mwaijungu alitumia fursa hiyo kuwaonya baadhi ya waumini na watu wengine kuacha tabia ya kueleza mambo yasiyo yajua tena bila kuwa na uhakika.
Alisema tabia hiyo huenda ndiyo iliyosababisha tukio la kukwama kufungwa kwa ndoa hiyo baada ya baadhi waumini na watu wengine kwa maslai yao walimua kueleza uzushi ulio iibua taaruki kubwa.
Baada ya nasaha hizo na kunukukuu baadkitakatifu cha Bihi ya maandiko kutoka kitabu Biblia ndipo ulipo fika muda kwa maharusi hao kutimiza ahadi ya kula kiapo cha uaminifu katika ndoa yao.

Comments