- Get link
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- Other Apps
MAKAMPUNI yaliyo chini ya mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Mehbub Manji, yamepewa saa 24 yawe yameondoka katika jengo la
PSPF PLAZA, zamani likijulikana kama Quality Plaza, vinginevyo yatang’olewa kwa
nguvu na kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart.
Notisi iliyotolewa
na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma – PSPF ambao ndio wamiliki
inataja kampuni zilizoko kwenye jengo hilo katika Kitalu Namba. 189/2 kwenye
Barabara ya Nyerere kuwa ni Quality Group Company Limited, Gaming Management
Limited, Q Consult Limited, Quality Logistics Company Limited na International
Transit Investment Limited, ambazo ziko chini ya Manji.
Uamuzi wa
kuyatimua makampuni ya Manji, Diwani wa Mbagala Kuu jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa
klabu ya Yanga, unafuatia uamuzi wa shauri lililokuwa katika Mahakama Kuu
Kitengo cha Ardhi ambao ulitolewa na Jaji Mgetta Novemba 24, 2016, ambapo
pamoja na mambo mengine, iliamuliwa kampuni hizo ziondoke mara moja.
"Katika
shauri husika, Mahakama iliamuru miongoni mwa mambo mengine, kuondoka mara moja
kwenye eneo husika linalojulikana kama PSPF Plaza, zamani Quality Plaza,
lililoko kwenye Kitalu Namba. 189/2 kwenye Barabara ya Nyerere. Unatakiwa uwe
umeondoka kwa amani katika muda wa saa 24 kuanzia tarehe ya notisi hii. Zingatia
kwamba, kama hutaondoka katika muda wa saa 24, Mfuko umemwagiza dalali Yono
Auction Mart and Co. Ltd kukuhamisha kwa nguvu," imeeleza notisi hiyo ya
Desemba 2, 2016 kwenda kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Quality Group of Companies.
Manji kwa
sasa ni mshauri wa makampuni ya Quality Group baada ya kujiuzulu rasmi
uenyekiti mnamo Julai 15, 2016.
Comments
Post a Comment