Featured Post

MAISHA YA WATU NA RASILIMALI WALIZOPEWA NA MWENYEZI MUNGU

Baadhi ya akina mama wa Kijiji cha Ikonongo wilayani Kishapu, wakitoka Kliniki, ambapo baiskeli ni chombo kikuu cha usafiri katika wilaya hiyo.
#BMGHabari
Upendo Hotel ni moja ya hoteli kubwa zilizoko katika Kijiji cha Nyenze wilayani Kishapu.
Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Kihapu wakimuaga mwandishi wa habari hii (hayupo pichani).

Baadhi ya wakazi wa vijiji vinavyozunguka na mgodi wa almasi katika wilaya ya kishapu mkoani shinyanga, wameelezea kutoridhishwa na uwepo wa wawekezaji wa madini katika wilaya hiyo kutokana na mchango wao mdogo kwenye shughuli za kimaendeleo.

Wakizungumza na Lake Fm, wakazi hao wamesema bado vijiji vingi wilayani kishapu vinakumbwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa huduma za afya, maji, miundombinu ya umeme pamoja na barabara, na kwamba wajibu wao kimaendeleo umekuwa mdogo ikilinganishwa na neema ya madini iliyopo katika wilaya hiyo.

Akizungumzia wajibu wa wawekezaji hususani wa madini katika maeneo mbalimbali nchini, Mwanasheria kutoka Taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora ADLG, Carolina Tizeba, amesema sheria ya madini ya Mwaka 2010, kifungu cha 10 inawataka wawekezaji kuwajibika kwa ajili ya maendeleo ya jamii kwenye maeneo waliyowekeza.

USIKOSE KUFUATILIA MAKALA YA "MAISHA YA WATU NA RASILIMALI WALIZOPEWA NA MWENYEZI MUNGU" HIVI KARIBUNI, KUPITIA 102.5 LAKE FM MWANZA NA BMG HABARI.

Comments