Featured Post

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHIMIZA MATUMIZI YA TAKWIMU SAHIHI ILI KUHARAKISHA MAENDELEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, (aliyevaa joho jekundu), akiwa nje ya Ofisi Kuu ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kilichoko Changanyikeni Jijini Dar es salaam, wakati wa Mahafali ya Pili ya Chuo hicho ambapo wahitimu 154 kutoka nchi nane Barani Afrika wametunukiwa Astashahada na Shahada za Takwimu Rasmi zinazotolewa na chuo hicho.


Na Benny Mwaipaja
MAKAMU wa Rais Mama SAMIA SULUHU HASSAN, amesema kuwa matumizi sahihi ya takwimu zilizokusanywa kwa njia ya weledi mkubwa yanaweza kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kasi zaidi Barani Afrika,
Mama Samia ametoa kauli hiyo leo wakati akiwatunuku astashada na shahada  wahitimu 154 kutoka nchi saba za kiafrika ikiwemo Tanzania, wakati wa Mahafali ya Pili ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kilichoko Changanyikeni Jijini Dar es salaam.
Amewataka wahitimu hao kutumia elimu na ujuzi walioupata katika chuo hicho kufanya utafiti rasmi na wenye viwango ili nchi wanachama walioanzisha chuo hicho waweze kutumia takwimu sahihi kupanga mipango yao ya maendeleo itakayosaidia kuwaondolea umasikini wananchi wake
Pause Mhe. Samia Suluhu Hassan-Makamu wa Rais-Tanzania
Aidha, amewahakikishia wahitimu kutoka Tanzania waliomaliza masomo yao katika chuo hicho kwamba serikali itawapatia ajira ili kuongeza kada ya wasomi waliohitimu mafunzo ya takwimu rasmi ili kuchochea maendeleo ya nchi
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amesema kuwa  Tanzania inatekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa ambapo moja ya mambo yatakayosaidia kufanikisha mpango huo ni matumizi ya takwimu rasmi na sahihi na kuwataka wahitimu kutoka Tanzania kusaidia kufanikisha nchi kuwa nchi ya viwanda.
Pause
Mkuu wa Chuo hicho kilichoanzishwa miaka 51 iliyopita, Profesa Innocent Ngalinda, ameiomba serikali ya Tanzania na nchi wanachama walioanzisha Taasisi hiyo ya elimu ya juu ya Takwimu Rasmi, kuijengea uwezo ikiwemo miundombinu ya majengo pamoja na wakufunzi ili kiweze kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu hiyo muhimu
Pause
Akitoa neno la shukurani kwa mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa Dkt. Albina Chuwa, amesema serikali imejipanga kutumia wataalamu wa takwimu Rasmi waliobobea walioko serikalini na katika sekta binafsi kufanikisha utafiti wa sekta ya viwanda unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Pause
Wahitimu wa Mahafali ya Pili katika Chuo hicho cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wametoka katika nchi za Nigeria, Ghana, Ethiopia, Somalia, Uganda, Liberia, Rwanda na wenyeji Tanzania.

Comments