Featured Post

MACHINJIO DODOMA YAKIMBIWA NA WACHINJAJI, WATEJA



By Habel Chidawali, Mwananchi
Dodoma. Wateja wakiwamo wawekezaji kutoka nje wameamua kuyakimbia machinjio mjini Dodoma na kuhamia mitaani kufanya shughuli hiyo.
Machinjio hayo yanayomilikiwa kwa ubia kati ya Serikali yenye hisa asilimia 49 na mwekezaji anayemiliki hisa asilimia 51, yalikuwa yakitumiwa na wawekezaji 13 wanaochinja na kusafirisha nyama nje lakini sasa wamebaki wawili.

Idadi ya mifugo inayochinjwa hapo pia imepungua kutoka mbuzi 1,200 kwa siku hadi 500, huku idadi ya ng’ombe ikipungua kutoka wastani wa 200 kwa siku hadi 30.
Chanzo cha kukimbia wateja na wawekezaji kimetajwa kuwa ni utitiri wa kodi zinazotozwa na Serikali kwa watu wanaochinja na kusafirisha nyama nje na hata watumiaji wa ndani.
Uzalishaji wa machinjio hayo, Hamisi Kissoyi amesema kuwa hali ni mbaya hivyo wameamua kupunguza wafanyakazi kutokana na uchumi kuyumba  jambo lililosababisha idadi ya wateja kuwakimbilia.
Amezitaja kodi zinazotozwa kwa mtu aliyenunua mfugo akitaka kusafirisha nyama ni ya awali mnadani (primary), kodi ya kwenye soko (secondary), machinjio,  ya wizara, Bodi ya Nyama na ya usafirishaji.
Mfanyabiashara wa bucha ya nyama mjini Dodoma, Andrew Bogobo amesema hawezi kupeleka ng’ombe kwenye machinjio hayo kutokana na gharama zinazotozwa kuwa kubwa.
CHANZO - MWANANCHI

Comments