Featured Post

TOA MAONI, BORESHA MUSWAADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI

Na Mwandishi Wetu
Mwanadamu katika maumbile yake amejengeka katika falsafa ya kufafuta ukweli na kuupambanua na taarifa zinazokinzana na ukweli wa wenyewe wa jambo fulani. 

Katika kutafuta ukweli, wapo watakaoamini, wapo ambao watakuwa hawaamini na wapo ambao hawapo kwenye kuamini wala kutokuamini.
Hivi karibuni mwezi Septemba mwaka huu, ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulisomwa Muswada wa Huduma za Habari 2016 nchini kwa mara ya kwanza ambao unalengo la kuifanya tasnia ya habari kupewa hadhi yake na kutambulika kuwa taaluma kamili. 

Kabla ya kusomwa na kujadiliwa Bungeni kwa mara ya pili na ya tatu, ni jukumu la wananchi, wadau wa habari wakiwemo wamiliki wa vyombo vya habari na taasisi nyinginezo ambazo kwa namna moja au nyingine wamekuwa wadau habari kutoa maoni yao ili kuufanya muswada huo uweze kuwa na matunda ya sheria ambayo itakuwa na manufaa kwa wananchi na wadau wote wa habari.

Nachelea kusema wadau hao wa habari hawajashirikishwa ipasavyo, kwa mujibu wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Peter Serukamba (Mb) zaidi ya asilimia 90 ya maoni ya wadau yamezingatiwa katika Muswaada huo ambao unatarajiwa kuwa sheria kamili baada ya kusomwa kwa mara ya pili na ya tatu Bungeni na hatimaye kupelekwa kwa Mhe. Rais wa Tanzania kuuridhia na kusaini ili uwe sheria kamili uanzae kutumika kwa maslahi ya taifa na wadau wa habari ndani na nje ya nchi.

Ni dhahiri Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii ndio yenye ushahidi wa wazi na wa nyaraka zinazoonesha kuwa wadau wakuu wote walishiriki katika hatua za ndani ya Serikali kutoa maoni na sasa wataendelea kushiriki zaidi katika hatua hii ya kabala ya Bunge kufanya kazi yake ya kisheria ya kutunga sheria, hakika sehemu kubwa ya maoni ya wadau yameingizwa katika muswada huo ambao bado wanapokea maoni zaidi maoni ya wadau ili kuufanya muswada kuwa bora na wenye tija nchini.

Nitumie fursa hii adhimu kuwaasa wadau wate wa habari nchini na nje ya nchi, kutumia nafasi iliyopo ya wiki moja zaidi na Mwenyekiti wa Kamati Bw. Serukamba baada ya muda wa kawaida wa kutoa maoni uliopangwa na Bunge kuisha muda ambao wananchi na wadau wa habari walipaswa kuusoma Muswaada wa Huduma za Habari 2016 unaolenga kuifanya tasnia ya habari kuwa bora zaidi kuliko hapo awali.

Kwa kufanya hivyo utakuwa si mtazamaji na wala mlalamikaji na kukesha kwenye mitandao ya kijamii na badala yake  utakuwa umetumia muda wako vizuri kutuma maoni yako kwa Kamati husika ya Bunge ili yafanyiwe kazi yaweze kufanya maboresho yatakayosaidia kupata sheria ya habari ambayo ni bora zaidi.

Wasilisha sasa maoni yako kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 kwa barua pepecan@bunge.go.tz, timiza wajibu wako maana hakuna haki isiyo na wajibu.

Ni jukumu langu mimi na wewe msomaji wa habari hii kutambua njia sahihi ya kutuma maoni yako ikiwa ni pamoja na kwenda mwenyewe kwenye kamati husika kueleza maoni yako hatua ambayo ni njia rahisi kwa wakazi wa Dodoma mjini na njia nyingine rahisi kwa watu wote ni barua pepe ikizingatiwa asilimia kubwa ya Watanzania wanatumia simu za kiganjani badala ya kulalamika tu kwenye mitandao ya kijamii. 

Zaidi ya hayo bado kuna watu wanachanganya jina la muswada huo, ukweli kwa Mujibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mtandao wake wa www.parliament.go.tz sehemu ya Miswada na Sheria jina sahihi ni “Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016” na sio “Muswada wa Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari wa mwaka 2016”.

Comments