Featured Post

PEP GUARDIOLA NDIYE KOCHA GHALI ZAIDI, ANALIPWA SHS. 60 BILIONI KWA MWAKA



 Manchester City itakuwa ikilipa mshahara wa Shs. 60 bilioni kwa mwaka kwa Pep Guardiola kuanzia msimu huu wa 2016-17.

MAKOCHA ni watu muhimu sana katika klabu yoyote ya soka na ndio pekee ambao hulaumiwa wakati timu inapofanya vibaya hata kama makossa ni ya wachezaji.
Kama Arsene Wenger alivyopata kusema “Makocha ni watu muhimu zaidi kwenye klabu na kama sivyo kwa nini wanafukuzwa wakati mambo yanapokwenda kombo.”

Makocha wanaleta falsafa zao kwenye klabu na wanaweza kubadili majaliwa ya timu na klabu zote kubwa ulimwenguni daima wanatafuta makocha bora zaidi bila kujali gharama.
 Pep Guardiola na Jose Mourinho wote wamejiunga na klabu za Manchester na ndio kwa kiasi kikubwa wanaongoza kwa kulipwa zaidi ulimwenguni. Pep Guardiola atakuwa akipokea kitita cha Pundi 15 milioni kwa mwaka (takriban Shs. 60 bilioni) kama mshahara wake katika klabu ya Manchester City katika mkataba wa miaka mitatu wakati Jose Mourinho ambaye pia ana mkataba wa miaka mitatu katika klabu ya Manchester United atakunja kitita cha Paundi 13.8 milioni (takriban Shs. 56.2 bilioni) kwa mwaka.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alisaini mkataba mpya wa miaka mitatu mwezi Mei 2014 utakaomfanya abakie Emirates kwa hadi mwisho wa msimu wa 2016-2017. Kocha huyo ambaye hivi sasa anawindwa na Chama cha Soka cha England ili anoe timu ya taifa ya nchi hiyo kuchukua nafasi ya Sam Allerdyce, kwa sasa analipwa kitita cha Paundi 8.3 milioni kwa mwaka (Shs. 33.2 bilioni). 
Ifuatayo ndiyo orodha ya makocha 20 wanaoongoza kupokea mishahara minono ulimwenguni katika msimu huu kuanzia Machi 2016:
1. Pep Guardiola (mkataba mpya) – Manchester City – Paundi 15 milioni (mkataba wa miaka mitatu kuanzia 2016-17)
2. Jose Mourinho (mpya) – Manchester United – Paundi 13.8 milioni (miaka mitatu na anaweza kuongeza)
3. Carlo Ancelotti (mpya) – Bayern Munich, Ujerumani – Paundi 9 milioni (mkataba wa miaka mitatu hadi 2019)
4. Arsene Wenger – Arsenal – Paundi 8.3 milioni (ulianza Mei 2014)
5. Zinedine Zidane – Real Madrid – Paundi 8 milioni (mkataba wa miaka miwili na nusu)
6. Jurgen Klopp – Liverpool – Paundi 7 milioni (mkataba wa miaka mitatu)
7. Antonio Conte (mpya) – Chelsea – Paundi 6.5 milioni (mkataba wa miaka mitatu kuanzia 2016-17)
8. Luis Enrique – FC Barcelona – Paundi 7 milioni
9. Mauricio Pochettino (mkataba mpya) – Tottenham – Paundi 5.5 milioni (mkataba wa miaka mitano utakaomfanya aendelee kubaki hadi 2021)
10. Unai Emery (mpya) – PSG – Paundi 5.65 milioni
11. Ronald Koeman – Everton – Paundi 6 milioni (mkataba wa miaka mitatu)
12. Rafael Benitez – Newcastle United – Paundi 4.5 milioni (mkataba wa miaka mitatu baada ya Newcastle kushuka daraja)
13. Diego Simone – Atletico Madrid – Paundi 4.4 milioni (mkataba wa miaka mitatu aliosaini mwaka 2015)
14. Massimiliano Allegri – Juventus – Paundi 3.50 milioni
15. Sam Allerdyce (mpya) – England – Paundi 3.50 milioni
16. Frank De Boer (mpya) – Inter Milan – Paundi 3.20 milioni
17. Claudio Ranieri – Leicester City – Paundi 3 milioni (aliboresha mkataba wake mwaka 2016. Akalamba kitita cha Paundi 5 milioni kama bonsai kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu)
18. Slaven Bilic – West Ham United – Paundi 2.95 milioni
19. Joachim Low – Ujerumani – Paundi 2.80 milioni
20. Tite – Brazil – Paundi 2.5 milioni
21. Walter Mazzarri – Watford – Paundi 2.5 milioni
22. Alan Pardew – Benfica – Paundi 2 milioni
23. Vincenzo Montella – AC Milan – Paundi 1.8 milioni
24. Rui Vitoria – Benfica – Paundi 1.5 milioni

Comments