Featured Post

BASATA YAMPONGEZA MUSTAFA HASANNALI KWA KUSHINDA TUZO YA UBUNIFU WA MAVAZI

                                                           National Arts Council BASATA
 Tarehe: 30/09/2016
  
BASATA Arts Centre                                                             
Tel. 2863748/2860485
 Fax: 0255- (022) – 286 0486                                                                                                                         
Ilala Sharif Shamba                                                                                                                                                                       
P.O. Box. 4779, Dar es Salaam
E-mail:basata06@yahoo.com

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lenye dhamana ya kufufua, kukuza na kuendeleza Sanaa nchini linapenda kuchukua nafasi hii kumpongeza msanii na mbunifu wa Mavazi Mustafa Hassanali kwa kushiriki kinyanga’anyiro cha Tuzo ya Mavazi ya Afrika Mashariki Kenya 2016 (Kenya Fashion Awards 2016) yaliyofanyika tarehe 03/09/2016 na kupata tuzo ya Mbunifu Bora wa Mwaka wa Afrika Mashariki.
 
Baraza linathamini mchango mkubwa wa Mbunifu huyu wa mavazi katika kuendeleza tasnia ya ubunifu, kwa kuanzisha Jukwaa la mavazi Afrika Mashariki na Kati, Swahili Fashion week na maonyesho mengine ya mavazi.

Aidha tuzo hii itakuwa chachu kwa ustawi wa tasnia ya ubunifu wa mavazi kwa kuwa imedhihirisha ubora wa kazi za sanaa za Kitanzania katika soko la Kimataifa. Baraza litaendelea kushirikiana na wabunifu wenye maono na bidii katika kukuza na kuendeleza sanaa nchini ili kuhakikisha sekta ya sanaa inasonga mbele kwani ni ukweli usiopingika kuwa tasnia ya sanaa ina mchango mkubwa katika kutoa ajira kwa watanzania wengi hususan vijana.

Baraza linatambua mchango wa Bwana Mustafa Hassanali katika kukuza maendeleo ya ubunifu na amekuwa akitoa fursa kwa wabunifu wengine wa Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Baraza linathamini na linatoa pongezi kwa Bwana Mustafa Hassanali kwa kazi nzuri anayoifanya.

SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI

Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI, BASATA


Comments