Featured Post

WANAFUNZI WA MTWARA GIRLS MABINGWA WA SAYANSI 2016



Mwanafunzi Angelus Albinus kutoka shule ya sekondari ya St. Joseph Kolping mkoani Kagera akionyesha drone yao waliyoitengeneza na mwenzake Adolph Tabaro. Wanafunzi hao walishinda tuzo Vernier Europe kutokana na ubunifu wao wa ‘The Use of a Spin-Electric Power Drone In Spying, Researching and Providing Optimal Security’.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wanafunzi walioshiriki maonyesho hayo.
 
Hili ndilo wazo la wanafunzi Mathias Kapenda na Jimmy Kibala kutoka shule ya sekondari Chidya mkoani Mtwara.
Mabanda ya baadhi ya wadhamini wa maonyesho hayo ya tano ya sayansi kwa wanafunzi nchini Tanzania.
  
Na Daniel Mbega

WANAFUNZI Nadhara Mresa na Diana Sosoka kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtwara (Mtwara Girls), jana waliibuka mabingwa wa taifa katika Mashindano ya Tano ya Sayansi ya wanafunzi wakati wa maonyesho ya siku mbili yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi hao ambao wazo la utafiti wao lilikuwa ‘Umaskini Siyo Suala la Msingi kwa Wanawake Mkoani Mtwara’ (Poverty Is No Longer An Issue For Women In Mtwara Region) waliwashinda wenzao 298 kutoka shule mbalimbali nchini Tanzania ambapo mbali ya kupewa nishani, tuzo kubwa na hundi ya Shs. 1.8 milioni, pia watadhaminiwa safari kwenda jijini Dublin, Ireland kuhudhuria maonyesho ya sayansi kwa wanafunzi wa huko (BTYSTE) yatakayofanyika Januari 2017.
Aidha, wanafunzi hao pia watapata udhamini wa shahada ya kwanza katika sayansi kutoka taasisi ya Karimjee Jivanjee Education Scholarships ya jijini Dar es Salaam.
Washindi wa pili kwenye mashindano ya mwaka huu ni Bennedict Msangi na William Kiluma kutoka Shule ya Sekondari Mzumbe ambao walikuja na wazo la ‘Umwagiliaji kwa Kutumia Mianzi Mzumbe’ (Bamboo Irrigation System in Mzumbe).
Washindi hao walipata nishani, tuzo na hundi ya Shs. 1.2 milioni.
Katika maonyesho ya mwaka huu, Morogoro ndiyo imeongoza kunyakua zawadi ambapo shule nne kutoka mkoani humo zilipata zawadi mbali mbali zikifuatiwa na shule tatu za Mtwara.
Arusha na Dar es Salaam zilipata zawadi mbili mbili kama ilivyokuwa kwa Zanzibar, Kagera na Simiyu wakati zawadi nyingine zilikwenda Katavi, Singida, Tanga, Mbeya, Shinyanga, Pwani na Kigoma.
Wadhamini wakuu wa maonyesho hayo, Kampuni ya BG Tanzania, nao walisema wataendelea kudhamini maonyesho yajayo ili kuweka hazina ya wataalamu wa sayansi wa kesho.
Zawadi nyingine kwa washiriki wa maonyesho hayo zilikuwa katika makundi manne ambayo ni Sayansi ya Baolojia na Ikolojia (Biological and Ecological Sciences) iliyodhaminiwa na Kampuni ya uchimbaji gesi ya Statoil kutoka Norway; Sayansi ya Kemia, Hisabati na Fizikia (Chemical, Mathematical and Physical Sciences) iliyodhaminiwa na Kampuni ya Simba Cement; Sayansi ya Kijamii na Kitabia (Social and Behavioural Sciences) iliyodhaminiwa na Shirika la Concern Worldwide; na Teknolojia (Technology) iliyodhaminiwa na Karimjee Jivanjee Foundation.
Katika makundi hayo, mbali ya kupatiwa medali na tuzo, washindi wa kwanza walipata Shs. 900,000, washindi wa pili Shs. 750,000 na washindi wa tatu Shs. 600,000 zikiwa ni ongezeko kubwa kulinganisha na mwaka uliopita ambapo mshindi wa kwanza alipata Shs. 500,000, mshindi wa pili Shs. 300,000 na mshindi wa tatu Shs. 200,000.
Aidha, wadhamini wengine wa maonyesho hayo walitoa zawadi mbalimbali ambao ni Songas, Taasisi ya Fizikia (Institute of Physics), Read International, Solaris, Karimjee Jivanjee, First Car Rental, Vernier Software & Technology, Tyndall, NCCA na Human Development Innovation Fund (HDIF).
Wadhamini wengine walikuwa ni SMK, Delfina, Dar es Salaam Serena Hotel, MMI Tanzania, Dar es Salaam Gymkhana Club, Coastal Aviation na DTP.

Wafuatao ni washindi wa tuzo maalum ambao pamoja na nidhani na tuzo, walipata vitita vya Shs. 450,000 kwa kila wazo lililoshinda:
Tuzo ya Kupenda Sayansi ya Songas: Moses Minja na Baye Manga Loyola High School jijini Dar es Salaam na utafiti wao ‘Automatic Attendance Taker’.
Tuzo ya Read International: Munira Abdallah na Imran Yusuf kutoka Mucechu Sekondari, Tanga na andiko lao la ‘Local Solution to Bleeding During Injuries’.
Tuzo ya Solaris: Hielonimo John na Vinord Matendo kutoka Kibaha Sekondari, Pwani na utafiti wao wa ‘Kubadili Sauti Kuwa Katika Nguvu ya Umeme’ (Conversion of Sound To Electrical Energy).
Tuzo ya Tyndall: Suleiman Sadik Khamis na Rahma Seleman Jumanne kutoka Mpendae Sekondari, Unguja na andiko lao la ‘The Harmonize Solar Oven’.
Tuzo ya First Car Rental: Julietha Johansen na Edina Alistides kutoka Shule ya Sekondari Bulyakashaju, Kagera na andiko lao la ‘Je, Utapiamlo ni Tatizo la Kiuchumi au Ujinga?’ (Is Malnutrition An Economic Or Ignorance Problem?).
Tuzo ya Vernier: Angelus Albinus na Adolph Tabaro kutoka St. Joseph Kolping, Kagera ambao walikuja na utafiti wao wa ‘The Use of a Spin-Electric Power Drone In Spying, Researching and Providing Optimal Security’.
Tuzo ya HDIF: James James na Michael Nandi kutoka Mbeya Sekondari na andiko lao la Electric Wheel Chair For Disabled. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa tuzo hiyo kwenda Mbeya Sekondari ambao mwaka 2015 Tunu Ngajilo na Ally Salum waliitwaa kutokana na utafiti wao wa Automatic Irrigation System.
Tuzo ya NCCA: Eliah Uledi na Andrew Magoma kutoka Masanga Sekondari, Kigoma na andiko lao la ‘The Survivorship Of Street Children In Kigoma Municipality’.
Tuzo ya Taasisi ya Fizikia (IoP): Gwakisa Gwakabale na Hapiness Katani kutoka Misunkumilo, Katavi na andiko lao la ‘To Investigate The Relationship Between The Expansion of Bimetallic Strip and The Bell Ring by Electric Current’.

Washindi wa makundi mbalimbali:
Sayansi ya Baolojia na Ikolojia:
1. Esther Paschal na Agape Mwalimu kutoka Ndwika Sekondari, Mtwara na utafiti wao wa ‘The Use Of Sweet Basil Plant To Prevent Mosquitoes’.
2. Jackson Nyiga na Victor Magita kutoka Ilboru Sekondari, Arusha na utafiti wao wa ‘Management Of Organic Food Waste’.
3. Doreen Ikula na Rose Rwegasira kutoka Kilakala, Morogoro na utafiti wao wa ‘Cholera In Morogoro Municipality’.

Sayansi ya Kemia, Hisabati na Fizikia:
1. Blandina Edmund na Johari Abubakar kutoka Chamaguha Sekondari, Shinyanga ambao utafiti wao ulihusu ‘Emulsifier Fro Increasing Life Span Of Milk’.
2. Claudia Laurent na Sheila Seif kutoka Dk. Salmin Amour Sekondari, Singida na utafiti wao wa ‘Does Fruits Lose Or Gain Vitamin C After Being Picked?’
3. Mathias Kapenda na Jimmy Kibaja kutoka Chidya Sekondari, Mtwara na wazo lao la ‘Kwa Nini Tetemeko la Ardhi Linatokea Katika Mabara Mengine na Siyo Bara la Afrika’ (Why Earthquakes Occur Mostly In Other Continents Than African Continent?).

Sayansi ya Kijamii na Kitabia:
1. Anna Apopolynary Ngairo na Getrude Deogratius Makoye kutoka Debrabant, Dar es Salaam na utafiti wao wa ‘The Use Of Local Resources In Teaching To Make Primary School Pupils Like and Apply Science’.
2. Shabani Mtoi na Munira Juma kutoka Morogoro Sekondari na andiko lao la ‘Can Discipline Be Managed In Order To Improve Academic Performance In Secondary Schools?’
3. Annastazia Michael na Dotnatha Ntunga kutoka Ifakara Sekondari na utafiti wao wa ‘Assessing The Effects Of Drug Abuse To Human Being and How To Reduce It’.

Teknolojia:
1. Rashida Remtula Kassu na Luteiya Ahmed Zubeir kutoka Kiembesamaki, Unguja na utafiti wao wa ‘Ultrasonic Frequency Against Flies’.
2. Joshua Mussa na Lucy Konyaki kutoka Binza Sekondari, Simiyu na utafiti wao wa ‘Mashine Rahisi ya Kutotolesha Vifaranga Katika Nchi za Dunia ya Tatu’ (Simple Egg Incubator For Third World Countries). Wanafunzi hao pia walipata Tuzo ya Udhamini (scholarship) wa shahada ya kwanza kutoka taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation.
3. Nancy Godfrey na Grace Temu kutoka Edmund Rice Sinon, Arusha na utafiti wao ‘A Low Cost Vegetable Cutting Machine’.


Comments