Featured Post

UJENZI WA MABANDA BORA YA SUNGURA



Hiki ni kizimba bora ambacho kinaonyesha kwamba juu kuna kizimba cha kuishi na chini ni kwa ajili ya sungura kucheza. 
Na Daniel Mbega
MPENDWA mjasiriamali, utakumbuka kwamba katika mfululizo wa makala hizi za ufugaji wa sungurakibiashara tumejifunza mambo mbalimbali ikiwemo uanzishwaji wa biashara hiyo ya mifugo, faida zitokanazo na ufugaji huo pamoja na aina mbalimbali zasungura wanaofaa kufugwa kwa matumizi mbalimbali.
Katika makala haya, tunaangalia namna ya ujenzi wa mabanda bora ya sungura ili wakuletee faida katika kipindi ambacho kuna mahitaji makubwa ya nyama.

Huku tukiangazia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 ambayo inataka Watanzania wawe katika uchumi wa kati, pamoja na kuzingatia Maendeleo Endelevu ya Dunia yanayotaka kukomeshwa kwa umaskini pamoja na kuongeza upatikanaji wa chakula, biashara ya ufugaji wa sungura ni muhimu kuizingatia.
Najua faida ya mifugo kwa sababu nimezaliwa na kukulia katika mazingira ya ufugaji ingawa wakati huo hakukuwa na maendeleo kama ya sasa.
Leo hii ninapozungumzia fugaji wa sungura natambua kwamba uwekezaji huo unaweza kukuletea tija katika njia nyingi tu kama kuuza mkojo wa sungura kwenye maabara mbalimbali, kupata samadi kutokana na kinyesi chao ambacho pia hutumika kuzalishia mionyoo. Nyama, hata hivyo, ndiyo bidhaa kubwa na muhimu.
Kuna mambo mengi ambayo unapaswa kuyafahamu kabla ya kuanza ufugaji wa sungura. 
PATA MWONGOZO UTAKAOKUSAIDIA KATIKA UFUGAJI NA JINSI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI YAKIWEMO MAGONJWA.
WASILIANA NA DANIEL MBEGA KWA SIMU HII +255 656 331974 ILI UPATE NAKALA YAKO SASA KWA GHARAMA NAFUU KABISA YA SHS. 20,000/= TU!! … FUATA LINK HII UPATE MAELEZO ZAIDI.



Comments